Monday, February 12, 2018

TANZANIA INATUMIA DAWA ZILIZO SALAMA KWA UHAKIKA MKUBWA

WaziriAfya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mamlaka za Kudhibiti Chakula na Dawa Barani Afrika unaofanyika Jijini DaeEs Salaam na kuhudhuliwa na n chi zipatazo 17 za Afrika.
Dkt. Ndugulile akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuifungua mkutano huo.

Pichani Naibu Waziri Dkt.Ndugulile akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Bi.Agnes Kijo kwenye mkutano huo utakaofanyika kwa siku tano na kujadili mfumo wa pamoja wa kudhibiti ubora wa dawa barani Afrika.
Dkt.Ndugulile akifuatilia mada (mwasilishaji hayupo pichani) katika mkutano huo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi.Agnes Kijo akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano wa Mamlaka za Kudhibiti Chakula na Dawa Barani Afrika
Msimamizi wa kitengo cha Afya katika Shirika la Maendeleo ya Afrika (NEPAD) yenye makao makuu yake nchini Afrika ya Kusini Bi.Margareth Ndomondo akiongea wakati wa uzinduzi huo.Shirika hilo katika afya linasaidia kupunguza magonjwa yanayoikabili nchiza Afrika.
 
 


TANZANIA INATUMIA DAWA ZILIZO SALAMA KWA UHAKIKA MKUBWA

Na.WAMJW-DAR ES SALAAM

TANZANIA ni miongoni mwa nchi inayotumia dawa zilizo salama na ubora wa hali ya juu barani Afrika kutokana na udhibiti na umakini unaofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mamlaka wa Udhibiti na ubora wa dawa barani afrika unaofanyika jijini Dar es Salaam.

”Sisi kama Tanzania tunafanya vizuri sana katika udhibiti wa madawa yanayoingia,nataka niwathibitishie kwamba Tanzania dawa zetu tunazozitumia ni salama na zipo salama kwa uhakika mkubwa” alisema Dkt. Ndugulile



Aidha ,Dkt. Ndugulile alisema kuwa ongezeko la matumizi ya dawa ambayo hayana kiwango na kutumika katika mfumo wa tiba umeleta changamoto katika kuongeza gharama za matibabu nchini na barani Afrika

Kwa mujibu wa Dkt. Ndugulile amesema changamoto hizo zinasababisha wagonjwa wengi kukaa hospitalini,kuongeza gharama, kuathiri matokeo ya mgonjwa na hatimaye vifo pamoja na kuleta usugu wa dawa kwa kutumia dawa zisizo na kiwango

Hata hivyo Dkt. Ndugulile alisema mkutano huo utajenga utaratibu na mfumo wa pamoja wa kuona ni jinsi gani wanaweza kudhibiti matumizi ya madawa yasiyo na kiwango barani afrika.

“Nataka niwathibitishie Watanzania kwamba tuna dawa za kutosha na dawa zote zinazoingia zina ubora unaotakiwa,Taasisi yetu ya TFDA inatambulika Kimataifa, ina viwango vya Kimataifa na tumeboresha maabara zetu kuwa za kisasa na kutumika katika bara la afrika katika udhibiti wa madawa”. Alisema Dkt. Ndugulile.

Naye kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Bi.Agnes Kijo alisema mamalaka hiyo imejidhatiti katika masuala ya udhibiti wa dawa hivyo kupelekea mkutano huo kufanyika Tanzania

“Maabara yetu hivi sasa imewekewa vifaa vya kisasa ambapo mwaka huu wa fedha ilitengewa shilingi bilioni tano nukta moja kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa ajili ya maabara ya Dar es Salaam na kanda ya ziwa ambapo itasaidia kufanyiwa uchunguzi wa dawa katika ukanda uliopo na hivyo kutoa majibu kwa wakati na mamlaka kufanya maamuzi sahihi” alisema Bi. Kijo.

Mkutano huo ambao una lengo la kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali yanayo uhusiana na udhibiti na ubora wa dawa ambapo kumekuwa na changamoto za matatizo ya madawa yasiyo na kiwango umekutanisha nchi zipatazo 17 na utafanyika kwa siku tano.   

No comments: