Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kikumbaitale kata ya Kigongo wakiwa kwenye hafra fupi ya makabidhiano. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt,Allan Kijazi wakitia saini hati za makabidhiano. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akitoa hati kwa mwenyekiti wa Kijiji cha Mwelani. |
Na,Joel Maduka,Geita
Shirika la hifadhi ya Taifa (TANAPA) limedhamini ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu wa shule mpya ya sekondari ya Kikumbaitale iliyopo kata ya Kigongo pamoja na Boti yenye injini kwa kijiji cha Mwekani vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 99.
Akikabidhi miradi hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Geita mwenyekiti ya Bodi ya wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ameitaka jamii kuitunza miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi wa kata ya Kigongo hususan kijiji cha Kikumbaitale.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi alisema mradi wa vyumba vya madarasa umetekelezwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale kata ya Kigongo ambapo TANAPA ilitoa kiasi cha shilingi milioni 46 na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale wamechangia vifaa kama vile mawe,kokoto, mchanga , tofali na maji ambavyo vimekadkugharimu juml a ya shilingi milioni 6.
"Madarasa haya yatapunguza tatizo la upungufu wa vyumba kusomea ambalo lipo katika shule za sekondari ya Kigongo .Kukamilika kwa madarasa haya kutasaidia kuanzishwa kwa shule ya sekondari ya Kikumbaitale ikiwa ni sehemu ya shule ya Kigongo mpaka itakapopata usajili wa kudumu",alisema Kijazi.
Aidha Dkt. Kijazi alisema TANAPA imeamua kufadhili boti ya kisasa yenye injini na maboya ikiwa na thamani ya shilingi milioni 47 kwa kikundi cha kusimamia fukwe cha Mwelani (BMU) ya kijiji cha Mwelani kutokana ushirikiano wa kijiji hicho na hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo katika kupambana na uvuvi haramu ndani ya ziwa Viktoria “ ni kutokana na ushirikiano huo TANAPA kupitia hifadhi kisiwa cha Rubondo ilipokea na kupitisha maombi toka kwa wananchi wa kijiji cha Mwelanina kuwapatia mradi wa Boti, injini na maboya yake ambayo itatumika kufanya doria katika ziwa Viktoria.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel ameishukuru TANAPA kwa ufadhili wa miradi hiyo na kuahidi kuwa mkoa itasimamia vyema miradi hiyo na pia amewataka wakazi wa Chato kuendelea kutoa taarifa za kuhusiana na uvuvi haramu na kwamba wananchi wote kwa kushirikiana na viongozi kufanya msako wa nyumba hadi nyumba ili kubaini nyavu haramu ambazo bado hazijasalimishwa.
No comments:
Post a Comment