Friday, February 9, 2018

SERIKALI KULIPA MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA KUANZIA KESHO


IMG_0013
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (hawapo pichani)  kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa (Picha-Wizara ya Fedha na Mipango)
IMG_0021
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (hawapo pichani) kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo Bw. Richard Mkumbo (Picha-Wizara ya Fedha na Mipango)
IMG_0030
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (Hawapo Pichani)kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo, Bw. Richard Mkumbo (Picha-Wizara ya Fedha na Mipango)
…………………………………………………………………………….
TAARIFA YA WAZIRI WA FEDHA KUHUSU MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI
Ndugu Wawakilishi wa vyombo vya habari, nimewaiteni leo hii ili niwape taarifa fupi kuhusu malipo ya madai ya malimbikizo ya mishahara kwa Watumimishi wa umma waliokuwa na madai ili muweze kuufikishia umma wa Watanzania.
Serikali kupitia mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management Information System – HCMIS) kufikia tarehe 01 Julai 2017 ilikuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara yenye jumla ya shilingi 127,605,128,872.81 kwa watumishi 82,111 Wakiwemo walimu 53,925 waliokuwa wanadai shilingi 53,940,514,677.23  sawa na asilimia 42.27 ya madai yote,   na wasiokuwa walimu 28,186 waliokuwa wanadai jumla ya shilingi 73,664,614,195.58 sawa na asilimia 57.73 ya madai yote. Madai haya yalikuwa ya muda mrefu mengine yakiwa ya kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2017
Madai haya yalijumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa mishahara.
MATOKEO YA UHAKIKI WA MADAI YA SHILINGI BILIONI 127,605,128,872.81 KWA WATUMISHI 82,111
  1. Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya shilingi  43,393,976,807.23 ikiwa ni asilimia 34 ya madai yote ya shilingi bilioni 127,605,128,872.81  yaliyohakikiwa yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.
  1. Madai yanayostahili kulipwa yanajumuisha shilingi bilioni 16.25 kwa walimu 15,919 na shilingi bilioni 27.15 kwa watumishi wasiokuwa walimu  11,470
  1. Madai yote yaliyoonekana kuwa sahihi ya shilingi bilioni 43.39 yatalipwa pamoja na mshahara wa mwezi Februari 2018 kwa mkupuo mmoja. Malipo ya Madai haya ambayo mengine yana zaidi ya miaka kumi majina ya walipwaji wote yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari, 2018.
Kwa matokeo hayo ya uhakiki, mazoezi yaliyofanyika likiwemo  zoezi la kuwaondoa kwenye Mfumo wa malipo ya mshahara (“payroll”) watumishi hewa, vyeti feki na wasio kuwa na sifa na  uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara uliofanyika limeweza kuokoa jumla ya shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na asilimia 66 ya madai yote ya malimbikizo ya awali ya shilingi bilioni 127.61 yaliyokuwa kwenye mfumo ambazo bila zoezi  la uhakiki kufanyika zingelipwa wakati zilikuwa hazistahili kulipwa.
Serikali itaendelea kulipa madai ya watumishi kadiri yanavyojitokeza ili kuondokana na malimbikizo ya aina hii ambayo yanaweza kuisababishia Serikali hasara kwa kulipa madai yasiyostahili.

No comments: