Thursday, February 8, 2018

MTULIA ASEMA SHIDA ZA WANANCHI KINONDONI NI ZAKE, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MGOMBEA ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdallah Mtulia ameendelea kuomba kura huku akiwaambi wananchi yeye hana tofauti na wao.

Pia shida za wananchi ni shida zake, matatizo yao ni matatizo yake pia na kuongeza yeye in mtoto wa kimaskini.tulia amesema hayo kwa nyakati tofauti kwenye mikutano yake ya kampeni kwenye uchaguzi huo wa jimbo hilo.Hata hivyo wakati Mtulia akiomba kura  kwa wananchi hao wa Kinondoni, mgombea ubunge wa Chadema Salum Mwalimu naye ameendelea kuomba kura.

Mwalimu amekuwa akitoa Sera mbalimbali zenye lengo kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo na kwamba anaamini yeye ndio mgombea sahihi ,hivyo wamchague alete maendeleo.Wakati wagombea hao kila mmoja akiomba kura  za wananchi hao ,kwa Mtulia yeye ameendelea kusisitiza changamoto za jimbo hilo anazijua na anao uwezo wa kuzitatua.

"Niliguswa na matatizo yenu ya kubomolewa nyumba nikaenda Mahakamani kuzuia bomoabomoa nikafanikiwa."Nilipambana kuhakikisha watu waliobomolewa wanapata hifadhi Magomeni. Nimekuja CCM kuhakikisha hilo linatimia," amesema Mtulia. Ameongeza kuwa "Niliacha ubunge, mshahara, posho na kiinua mgongo changu kwa sababu nawajali wana Kinondoni. Ukiwa jiongozi wa upinzani hauwezi kufanya lolote.

"Maendeleo hayapatikani kwa kutukana, kukashifu, matusi. Maendeleo huja kwa ushirikiano na mahusiano mema," amesema.Amefafanua zaidi  ni kweli anampenda Rais,Dk.John Magufuli  na kuuliza ataachaje Rais ambaye anajenga reli ya kisasa, kununua ndege za kisasa, ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme. Rais mkweli na muwazi.

Ameongeza atashirikiana na Meya na Mkurugenzi kugawa maeneo ya Mabwepande kwa ajili ya wana Kinondoni waliobomolewa nyumba."Mchague Mtulia arudi Bungeni kivingine akiwa Mtekelezaji wa ilani ya uchaguzi inayoongoza dola," amesema Mtulia.Amesena akishinda atahakikisha vijana wanakopeshwa Pikipiki na akina Mama wanapewa mikopo ya biashara.

"Nikishinda nitahakikisha Zahanati ya Makumbusho inajengwa, fedha zipo."Nikishinda nitahakikisha kiingilio Hospitali ya Mwananyamala nakifuta, Wananchi wanapata Bima za Afya na Wazee wanapewa huduma bora,"amesema Mtulia.Pia atapunguza  mrundikano wa wagonjwa Hospitali ya Mwananyamala kwa kuhakikisha hospitali ya Mabwepande inakamilika ili kupunguza foleni, kujenga Maghorofa Hospitali ya Mwananyamala.

Amewaaambia wananchi wa jimbo hilo atahakikisha kupatikaba kwa njia mpya ya usafiri kutoka Makumbusho Mpaka Muhimbili, Makumbusho mpaka Posta."Tatizo la taka litakuwa bistoria. Nitahakikisha tunajenga kiwanda cha taka pale Mabwepande, pesa zipo."Kwa wale vijana wenye vipaji, nitashirikiana na Msanii Diamond Platnum kuhakikisha tunaunda timu itakayohakikisha inaibua, inakuza na inalinda kazi za Wasanii wa Kinondoni," amesema.

 Ameongeza maji hayatoki mara kwa mara lakini bili inayotoka ni kubwa, hivyo akishinda atakaa meza moja na Waziri na Dawasco kurekebisha hali hii mbovu iwe historia."Nimetoka kule na kujiunga na CCM ili niweze kupata nguvu ya kuwatumikia wakazi wa jimbo la Kinondoni."Nawaombeni sana itakapofika Februari 17 mkanipigie kura za ndiyo. Kumchagua Mtulia ni kuchagua maendeleo," amesema  Mtulia
MGOMBEA ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdallah Mtulia ameendelea kuomba kura huku akiwaambi wananchi yeye hana tofauti na wao.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni jana jioni katika viwanja vya Vegas,Makumbusho,Kinondoni jijini Dar.
Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika kwenye kampeni katika viwanja vya Vegas,Makumbusho Kinondoni jijini Dar
Baashi ya Wananchi wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kampeni hizo.

No comments: