Monday, February 12, 2018

MTANGAZAJI LIKUDA AHAMIA A.FM RADIO

 Meneja mkuu wa A.fm Radio Tatenda Nyawo (kushoto)akiwa kwenye picha ya pamoja na mtangazaji  Emmanuel Likuda mapema leo,baada ya mtangazaji huyo kutambulishwa rasmi kwa wasikilizaji kama mtangazaji wa kipindi cha Amka Tofauti kinachorushwa na A.FM
  Likuda kwenye picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha  Amka Tofauti  Victor Simon na Elizabeth Kachenje. 
 Mtangazaji Likuda akiwa na watangazaji wa kipindi cha  Amka Tofauti,kushoto ni  Victor Simon,Elizabeth Kachenje na msimamizi wa Vipindi Ally Mohamed (Kulia)Mtanganzaji mkongwe nchini Emmanuel Likuda,leo amejiunga rasmi na A.FM RADIO kama mtanganzaji akijikita zaidi katika kipindi cha Amka tofauti.

Akiongea wakati wakumtambulisha Likuda kwa wasikilizaji,Meneja mkuu wa A.FM Bw. Tatenda Nyawo amesema,hiyo ni zawadi maalum na upendo kwa wasikilizaji wa a.fm 92.9 Dodoma,hasa katika msimu huu wa siku kuu ya Wapendanao (VALENTINES).

Bw.Tatenda ameongeza kuwa Likuda ni mtangaji mwenye uzoefu wa kutosha katika masuala ya utangazaji,hivyo kujiunga kwake na Af.m ni njia moja wapo ya kukipeleka kitu hicho katika hatua nyingine,kama ilivyo kauli mbiu ya A.fm kwa mwaka huu ‘’2018 level Nyingine”.

Kwa upande wake Likuda amesema ni furaha sana kujiunga na A.fm na kutokana na uwezo na uzoefu alionao,ana Imani kuwa A.fm itasonga mbele Zaidi katika kutimiza dhima yake kwa jamii hasa wakazi wa Dodoma na kwamba vipo vitu vingi ambavyo amejipanga kuvitoa kama zawadi kwa wasikilizaji wa A.FM kupitia kipindi cha AMKA TOFAUTI ambacho hurushwa kila siku kuanzia JUMATATU- IJUMAA saa 11:00 Mpaka saa 03:00 Asubuhi.

Likuda alianza safari ya utangazaji mwaka 2004 baada ya kumaliza chuo cha Africa college of management,ambapo uamuzi wa kusoma chuo hicho ulikuja baada ya kuvutiwa na watangazaji wakubwa aliowasikia katika enzi zake.

Baada ya kumaliza chuo, mwaka 2004, alifanikiwa kuanza kazi ya utangazaji katika kituo cha c2c ambapo aliweka historia ya kuwa mtangazaji wa kwanza kurusha kipindi cha uchambuzi wa filamu kilichoitwa filamu na wasanii.

Kipindi hiki, likuda alishiriki kuratibu matamasha makubwa kama la joe thomas, chingy, beenie man, tanya stevens na wengineo,na baadae likuda alijiunga na Cloudsfm kama mtayarishaji wa kipindi cha jahazi na hatimaye kuwa mtangazaji wa kipindi cha jahazi.

No comments: