Sunday, February 11, 2018

Meya Mwita aungana na wananchi jiji la Dar es Salaam kupima magonjwa ya Kisukari,Presha.

 Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akijiandaa  kupima Kisukari leo aliposhiriki kongamano la kupima Magonjwa ya Kisukari na Presha .
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata kipimo cha Presha kutoka kwa Dokta Mahmod Shahamati ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Iranian kilichopo jijini hapa.

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo ameungana na wakazi wa jijini hapa katika kongamano la  kupima Magonjwa ya Kisukari na Presha lililoandaliwa na Lions Clubs International kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha Irania  kilichopo jijini hapa.

Katika kongamano hilo Meya Mwita amewapongeza waandaaji  na kuwaeleza kuwa wasiishie hapo hivyo wafikishe huduma hiyo kwenye halmashauri nyingine za jiji la Dar es Salaam ili wananchi wote waweze kupata huduma hiyo.

Meya Mwita amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kucheki afya zao hususani inapojitokeza fursa hizo kwa kuwa baada ya kupata majibu ya vipimo hivyo inawapa urahisi katika kupata matibabu.Amesema Taasisi hizo zimekuwa na mchango mathubuti  kwa wananchi kutokana na uzalendo mkubwa waliokuwa nao na hivyo kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo.

"Jambo hili ni muhimu sana, ninawapongeza, ombilangu kwenu, angalieni namna ya kuendelea kuwasaidia wananchi wengine katika jiji letu la Dar es Salaam, huduma hii ni ya muhimu sana na kila  mwananchi anahitaji kuipata" amesema Meya Mwita.

Awali akimkaribisha Meya Mwita, Rais wa Lions Clubs Shaheen Alam amempongeza na kumueleza kuwa  wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha  Iranian kwa lengo la kuwasaidia wananchi kutambua afya zao.

Imetolewa leo Februali 11 na  Christina Mwagala Afisa Habari Ofisi ya Meya wa Jiji. 

No comments: