Tuesday, February 6, 2018

LESENI MADUKA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI KAA LA MOTO

*Maduka yamepungua,baadhi ya wamiliki waingia mitini
*Kati ya maduka 297 ya awali sasa yamebaki 70,matawi 40
*BoT yaendelea kuchambua leseni za maduka 65, 

Na Said Mwishehe,Blogu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT)imesema wakati mchakato wa kutoa upya wa leseni kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ukiendelea, maduka yaliyokidhi vigezo hadi sasa ni 71 na matawi 40 kati ya maduka 297 yaliyokuwepo awali.

Juni mwaka jana, wamiliki was maduka hayo walitangaziwa kuwa wanatakiwa kuomba upya leseni za maduka ya kubadilisha fedha na hatua ilitokana na tuhuma mbalimbali za maduka hayo ikiwamo ya kwamba kuna baadhi ya maduka yanatumika katika utakashiji fedha.

Akizungumza mchakato kuhusu utoaji upya wa leseni kwa maduka hayo , Meneja wa Huduma za Fedha na Maduka ya kubadilisha fedha chini ya Usimamizi wa Idara ya Mabenki, Eliamringi Mandari amefafanua watatoa taarifa rasmi kuhusu mchakato huo.

Mandari wakati anatoa mada inayohusu kanuni mpya za usimamizi wa maduka ya fedha kwa waandishi wa habari waliopo kwenye semina iliyoandaliwa na BoT.Lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo wa taarifa sahihi zinazohusu uchumi,biashara na fedha,ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kati ya maduka hayo 297ni maduka 71 tu ndio yamekidhi vigezo.

"Naomba hapa tuelewane kwanza,mchakato wa kutoa leseni kwa maduka hayo ya kubadilisha fedha za kigeni bado unaendelea na utakamilika siku za karibuni na baada ya hapo tutatoa taarifa rasmi."Hii ambayo tunaeleza si kwamba ndio taarifa ya mwisho ila naelezea hatua ambayo tumefikia hadi sasa.Mchakato huo ulianza Juni mwaka jana na ulitakiwa kukamilika Desemba mwaka jana.

" Hats hivyo umechelewa kukamilika kwasababu wamiliki wa maduka wengi walileta maombi tarehe 29 ya Desemba mwaka jana.Hivyo tumefunga maombi ya leseni na kinachoendelea no kupitia maombi maduka 65 na tukimaliza ndio tutatoa taarifa rasmi,"amesema Mandari.

Akifafanua zaidi Mandari amesema hadi sasa maduka ambayo yamekidhi masharti na vigezo vilivyotolewa na BoT ni 71 pamoja na matawi 40.Wamiliki wengine wa maduka hayo wapatao 50 wameshindwa kuomba maana hawajasema chochote ila wameona wapo kimya.

"Maduka 297 ya kubadilisha fedha za kigeni ndio yalikuwepo lakini kutokana na mchakato unaoendelea wapo walioshindwa kutimiza vigezo vilovyowekwa.Matokeo yake maduka yaliyokidhi vigezo ni 71 na matawi 40,hivyo tunaweza kusema ni kama maduka 111," amesema Mandari.

Ameongeza kwa kuwa muda wa maombi ulishakwisha maana yake hata kama maduka 65 ambayo maombi yake ndio yanaendelea kupitiwa hata kama yote yatapita bado idadi ya maduka haitafikia ile ya mwanzo kwani yamepungua.Alipoukizwa maduka ambayo yamefungwa wameshindwa katika vigezo gani,amejibu wapo walioshindwa kwasababu ya kushindwa kuelezea mtaji wa fedha zao ,kwani wapo ambayo wamesema wamesema mitaji yao ilitokana na kuuza mali zao.

Pia wamiliki wengine wa maduka hayo wameshindwa kuelezea pesa zao zimetokana na mini kwani hata unapowauliza wapo wanadai wametoa fedha kwenye daladala lakini wanapoombwa wapeleke vielelezo wanashindwa.

Alipoulizwa je wamebaini uwepo wa maduka hayo kujihusisha na utakatishaji fedha,amejibu kuwa hawezi kulitolea majibu maana wanaohusika na hilo utakatishaji fedha ni taasisi nyingine.Kuhusu walioshindwa kuomba tena leseni ya maduka hayo wakati zamani walikuwa wanatoa huduma za kifedha amejibu ni ngumu kujua sababu kwani hajaomba tena ,ni kama vile wameingia mitini.

Hata hivyo ,Mandari amesema mchakato huo umesaidia Serikali kupata fedha maana wapo ambao waliianzisha maduka kwa kuuza mali lakini hawakuwa wamelipa fedha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

"Walipokuja kwetu tuliwaelekeza na hivyo wapo waliokwenda TRA kuchukua baadhi ya nyaraka na ili wazipate walitakiwa kulipa fedha ambazo mwanzoni hawakuwa wamelipa," amesema Mandari.

No comments: