HOSPITALI na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Katika kukabiliana na uhaba huu unaosumbua taifa , Exim Bank Tanzania, yenye uwepo wa kimataifa imeanzisha mradi unaolenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini kama sehemu ya kampeni yake yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii.

Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya, ni hospitali ya sita kupokea mchango huu, baada ya Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, Arusha mwezi uliopita, Hospital ya rufaa Dodoma mwezi Novemba, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka jana. Tukio lilifanyika kwenye hospitali hiyo wodi ya wazazi META na mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Dr. Godlove Mbwanji.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Bwana Stanley Kafu alisema, “ Benki ya Exim imekuwa ikisheherekea miaka 20 ya uanzilishi toka Agosti mwaka jana 2017. Kama ishara ya kushukuru watumishi wake na jamii kwa ujumla, benki imeanzisha mpango wa kutoa vitanda na magodoro kwa hospitali nchini kote kila mwezi. Benki itaendelea mpango huu kwa mwaka mmoja hadi Julai 2018. "
Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya rufaa ya Mbeya, Dr Godlove Mbwanji alipongeza Exim Bank Tanzania kwa ahadi yake ya kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye ma hospitali ambao unakabiliwa na taifa na kuleta juhudi zake kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya. Alisema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii san a sana kwenye wodi ya wazazi.”
Ikiwa kama sehemu ya mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” benki ya Exim itatoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali katika mikoa ya Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Shinyanga, Mtwara, Pemba na Unguja ambapo mpaka sasa Dar es Salaam, Unguja, Mtwara, Arusha, na Dodoma tayari wameshapokea misaada.
Katika kipindi cha miaka 20 ya kuwepo sokoni benki ya Exim imejenga taasisi imara kijiografia, katika bidhaa za kivumbuzi, mahusiano mazuri na wateja na uwezo wake wa kutoa huduma kwa haraka zaidi.
No comments:
Post a Comment