Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo akitoa maagizo kwenye ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri
ya Chamwino mkoani Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino
mkoani Dodoma.

Selemani Jafo akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamonga wakati
akitoa maelezo kuhusu eneo lililotengwa kwa ajili ya uboreshaji Kituo cha Afya
Chamwino.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kujionea eneo litakalotumika kuongeza
majengo ya Kituo cha Afya Chamwino.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua maendeleo
ya ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na
kuagiza Wakala wa Majengo(TBA)na Suma JKT kuangalia njia bora ya kulifanya
jengo hilo liweze kukamilika kwenye ubora unaotakiwa ili watumishi wahamie.
Watumishi wa Halmashauri hiyo kwasasa wanatumia
jengo la Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na jengo lao kutokamilika.
Jafo ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kukagua
utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mwezi Novemba mwaka jana, ambapo aliagiza
ujenzi huo ukamilike ifikapo Januari mosi mwaka huu.Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi huo, Jafo
amesema ameridhishwa na sababu zilizotolewa zilizofanya kukwama kukamilishwa
kwa jengo hilo.
“Jengo hili awali lilikuwa linajengwa na mkandarasi
mwingine lakini kutokana na utendaji wake kutoridhisha tuliamua kumpatia Suma
JKT na niliagiza jengo likamilike Januari mosi mwaka huu, lakini bado
halijakamilika,”alisema
Amesema sababu zilizotolewa ambazo mkandarasi
amekumbana nazo ameona ni vyema watumishi wakaendelea kuvumilia kutumia ofisi
ya Mkuu wa wilaya hadi hapo itakapokamilika kwenye ubora unaotakiwa.Waziri Jafo amewataka kuifanya tathmini hiyo na
kwamba kwa kuwa wanaelekea katika mipango ya bajeti wataangalia namna ya
kushirikiana na Halmashauri ili jengo liweze kukamilika.
Awali, Mkandarasi kutoka Suma JKT, Mhandisi David
Pallangyo amesema ukamilishaji umekwamishwa kutokana na hali ya hewa na pia
makosa yaliyofanywa na mkandarasi wa awali.“Hapa hii flow ya chini tuliona tuikamilishe lakini
hali ya hewa na hizi mvua maji yanajaa hivyo tunafanya tathmini kama tutaweza
ni vyema tukaweka water proof,”amesema
Aidha Mkandarasi Mshauri kutoka TBA, Mhandisi Vilumba
Sanga amesema wanafanya tathmini katika jengo hilo kuangalia namna ya
kulikamilisha kwa kushirikiana na Suma JKT.“Tunafanya ‘estimate’ ya water proof maana maji
yanajaa, hii inatokana na makosa yaliyofanywa na mkandarasi wa awali, huyu
mkandarasi wa sasa anakutana nayo site,”amesema Sanga
Katika
hatua nyingine, Waziri Jafo ametembelea Kituo Cha Afya
cha Chamwino Ikulu kuangalia uboreshaji wa kituo hicho ambacho kimeingiziwa
Sh.Milioni 500 kwa ajili ya kujenga Wodi ya akina mama na watoto, maabara,
Chumba cha Kuhifadhia maiti.
Hata hivyo, amekuta ujenzi huo haujaanza kutokana
na eneo linalotakiwa kujengwa kuwa dogo na hivyo kuahidi kufanya tathmini
halisi kwa kushirikiana na wataalam kuangalia uwezekano wa kujengwa jengo la
ghorofa.
No comments:
Post a Comment