Friday, January 19, 2018

USAJILI NDANI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU

Usajili katika kata za Uhuru, Ayamohe, Ayamami, Imboru, Silaloda umemalizika wilayani Mbulu huku wananchi wakimininika kuendelea na Usajili kwenye Kata za Daudi, Marang, Gidamba, Gehandu na Titiwi huhu vijana wakijitokeza kwa wingi baada ya kutambua umuhimu wake katika masuala ya Elimu.

Ndg. Prosper Alfred Marmo mkazi wa Kata ya Daudi Kijiji cha Moringa, Kitongoji cha Magasi amesema ameona ni vyema akatii agizo la Serikali ili apate Kitambulisho kitakachomtambulisha kupata huduma mbalimbali ikiwemo mikopo ya elimu ya juu pindi wakati utakapofika.

Akizungumzia zoezi la Usajili linaloendelea kwa sasa Wilayani Mbulu; Afisa Usajili Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bi. Amina Farijala amesema pamoja na kwamba msimu huu ni wakilimo na wananchi wengi wako kwenye shughuli za kilimo mwitikio wao umekuwa mkubwa hasa nyakati za mchana na hivyo kuwaasa kupanga vizuri shughuli zao ili kujitokeza kwa wingi nakwa wakati kusajiliwa.“ Mwitiko hawa wa kundi la wazee umekuwa mkubwa na kutumia moyo hasa tunapoona wazee wanafika kwenye vituo kusajiliwa” alisema

Kwa sasa NIDA inandelea na zoezi la Usajili kwa mikao 19 ya Tanzania Ikiwemo Manyara na inakusudia kufikia Desemba 2018 zoezi hili kuwa limemalizika nchi nzima na wananchi kuanza kutumia Utambulisho wao kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kimaendeleo.

Mzee Tarmo Naita wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu mkoani Manyara akiweka vidole katika mashine ya Usajili BVR ikiwa ni sehemu ya hatua ya pili ya Mwombaji kuchukuliwa alama za kibaiolojia.
Mzee Nayhan Hhando mwenye miaka 79 mkazi wa Kitongoji cha Ampe akipigwa picha kwa kutumia Mashine za Usajili Vitambulisho vya Taifa na Afisa Msajili Msaidizi wa NIDA Ndg. Pastori Silo.
Afisa Msajili Halmashauri ya Mji wa Mbulu Ndg. Amina Farijala akitoa maelekezo

Wananchi Kijiji cha Moringa Halmashauri ya Mji ya Mbulu wajitokeza Kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.
Wananchi Kata ya Daudi Halmashauri ya Mji ya Mbulu wakiwa wamepanga foleni tayari kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.
Ndg. Emmanuel Safari Amnaay mkazi wa Kitongoji cha Malasi (kulia) akiwa na Ndg. Josephati Faustini Masay mkazi wa Malasi kwa pamoja wakijaza fomu ya maombi ya Kitambulisho cha Taifa wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea.

No comments: