Tuesday, January 30, 2018

MAWAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO WA TANZANIA NA RWANDA WAKUTANA KUJADILI MRADI WA UJENZI WA RELI YA ISAKA- KIGALI



Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mkutano kuhusu upatikanaji wa Fedha za mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kuanzia Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda.
Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (kushoto) na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Eugene Kayihura (kulia) wakiwa katika majadiliano ya pamoja kabla ya kuanza kwa mkutano kuhusu namna ya kupata fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda.
Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (wa pili kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) ukiendelea kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (kushoto) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (kulia) wakiondoka baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na kutoka Rwanda ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakisaini maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakibadilishana taarifa walizosaini za maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji wa Fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango

………………………

Benny Mwaipaja, WFM


Mawaziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania na Rwanda wamekutana Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kupata fedha za Ujenzi wa Reli yenye Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa mikutano kuhusu suala hilo iliyoanza kuanzia Januari 20, 2018.

Katika Mkutano huo wamejadili kuhusu njia ambayo inaweza kuwa rahisi kupata fedha ikiwemo ya kutumia Sekta binafsi, Serikali kukopa au kumweka mwekezaji ambapo wamekubaliana kupitia upya taarifa zilizo wasilishwa mezani za pande hizo mbili na kufanya maboresho na pia kuzungumza na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa pamoja ili wakati wa kikao kijacho waweze kujadili suala hilo kwa kuangalia vigezo na masharti ya kupata fedha.

Kikao hicho ambacho ni cha watalamu kimewakutanisha Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri kutoka Rwanda Mhe. Gatete Claver pamoja na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura na Makatibu wakuu wa wizara hizo na wajumbe wengine.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaungaza, wamesaini maagizo hayo ya Mawaziri kwa ajili ya utekelezaji.

Ikumbukwe kuwa mapema mwezi huu Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikubaliana kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa Reli kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda na wakatoa maagizo ya kuanza utekelezaji kwa kuangalia namna ya kupata fedha za mradi huo.

No comments: