Thursday, January 18, 2018

JE.! WAZIJUA FAIDA LUKUKI ZA FENESI.?

Imeandaliwa na ​ Geofrey Chambua ​kutoka vyanzo mbalimbali

Huenda umewahi kuliona na kulipita tu ama kutovutiwa na ladha yake ama kukereka na utomvu wake baada ya kula

Habari mbaya kwako ni kwamba umekosa kitu adimu na maridhawa sana......Hili ni moja ya matunda yanayochukuliwa kama MFALME WA MATUNDA (The King of Fruits) kwa kuwa na karibu vitamin vyote muhimu yaani A, B1, B2 na C..

Na sehemu zinazotumika ni majani, matunda, utomvu, mizizi na magamba. Na mfenesi unaweza kukua hadi kufikia kimo cha mita 20.........na nakusihi sana kuanzia leo ujitahidi kula walau punje tatu tu na ukiweza hata mbegu zake kwa kadri ya mada hii

Leo nimejikuta tu nafukunyua tunda hili baada ya kulikuta mahali fulani na jinsi watu walivyokuwa wanatua kilich cha thamani ndipo nilipoanza kugoogle nikakuta faida na hata hilo jina la lugha ya malkia huitwa Jackfruit

Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu.
Hakuna anayejua vizuri asili ya mafenesi lakini inaaminika asili yake ni katika misitu ya mvua nyingi ya Magharibi ya ghats (western ghats). Lakini kwa sasa inalimwa katika nchi za india, Burma, Sri lanka, China, Malaya, East in indies, Qeens land, Maturities, Hawaii, Suriname, Brazil, Kenya, Uganda na Tanzania, Na nchini Tanzania hulimwa Pemba, Unguja, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga na Mbeya(Kyela) nk.

Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutubisho hivyo ni pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga na nyuzinyuz (fiber) ambazo husaidia kwenye mfumo wa mmeng'enyo na kuchagiza tatizo la kupata haja (constipation) na linasaidia pia kuzuiwa kuvimbiwa.

Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu (cholesterol). Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine kadha wa kadha,

Sukari ya Fenesi ni dawa ya sukari sumu mwilini kwa kuwa linasharabiwa taratibu mwilini na kufyonza sukari sumu na hii husaidia pia katika kuhibiti shinikizo la damu mwilini ( Jackfruit is more slowly absorbed into the bloodstream, which prevents sugar crashes, sugar cravings, and mood swings, They are well known because of its high potassium content. This helps the blood vessels relax and maintains proper blood pressure.)

Uwepo wa viondosha sumu ndani ya tunda hili kunasaidia pia kuongeza uwezo wa kuona. Tunda hili pia linatajwa kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya potassium yanayosaidia kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.

Wataalamu wa mambo ya afya wamezitaja faida nyingine za tunda hili kuwa ni pamoja na:

Kinga: Fenesi ni chanzo kizuri cha vitamini C. Uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo pamoja na viondosha sumu kunaongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini. Husaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi.

Nishati: Ni tunda salama kiafya, halina lehemu licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta. Pia, lina wanga na kalori kwa kiasi kikubwa. Sukari iliyomo ndani yake huchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mwili.

Wingi wa Vitamin A kwenye Fenesi husaidi kusharabu kwa nywele (jackfruit contains vitamin A to keep the hair moisturized through increased sebum production)

Hurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.

Asthma: Inasadikika pia kuwa tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu.

Si hivyo tu, fenesi lina vitamini muhimu katika utengenezaji wa damu mwilini na pia kusaidia kukupa usingizi mwanana na kukuepusha na mauzauza (Jackfruit has a high content of magnesium, a mineral that is directly linked to improving the quality, duration, and tranquility of sleep. Jackfruit also helps regulate the metabolism, to help reduce sleep disorders and the occurrence of insomnia)

MENGINE ZAIDI AMBAYO HAYASEMWI SANA KUHUSU FENESI

Kuna faida lukuki kwenye MBEGU ZA FENESI (6-remarkable-benefits-of-jackfruit-seeds)

kiboko zaidi ni ukizichoma hizo mbegu. Ni tamu sana na laini kama kiazi ila kuwa mwangalifu wakati wa kuchoma zikiiva wakati mwingine hupasuka na kutoa sauti kama ya mlipuko, sasa kama ulikuwa unasonga ugali kwenye jiko la kuni ukaweka mbegu mbili tatu kwenye moto ili uendee kugonga mdogomdogo ikipasuka hata moja ugali wote lazima ujae majivu na michanga na kama mwoga unaweza toka nduki vilevile....Ladha yake huwa inashahabiana na kiazi kitamu kilichochomwa na unachofanya ni kubandua gandale na kutafuna kokwale lililokwiva kwa moto...kuna jamii zinginea zinakula mbegu za fenesi na kuna jamii nyingine hawajui hata kama zinaliwa. Kuna some factors zinazofanya kitofautiana kwa resource kati ya jamii moja hadi nyingine......Tanga wanazichanganya na mihogo (muhogo wa aina ya kibanda meno au kitingisha ndevu maeneo ya Muheza) zinaungwa na nazi. Halafu ili ufaidi zaidi Mihogo iwe inawahi kuiva ile ya unga unga achana na ile chelema, mchanganyiko wake ni hatari sana (njoo chemba)

Utomvu wa fenesi ni dawa ya ngiri...ichukue hiyo kama ulikuwa hujui na pia husaidia kulainisha uso japo unahangaika na SCRUB za MJINI

Majani ya Mfenesi hutibu homa magonjwa ya ngozi majipu, vidonda na kisukari

Mibamiba ya fenesi wengine hugeuza chanuo panapo dharura na ikibidi

Faida nyingine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.

TANBIHI

kuna mada ambayo inaongelewa sana, nayo ni "kula fenesi na baadaye kunywa pombe kunaweza kukupelekea mauti."
Mtaalam wa masuala ya afya wa hospitali ya Puren ya Wuhan ameonya pia kuwa hoja hiyo ina uhalali kisayansi.

Wakati nikibarizi kwenye mitandao mbali mbali ya habari niliweza kukutana na habari hii ambayo imekuwa kichwa cha habari nchini hapa "Wataalam wa Chuo cha Tsukuba, nchini japan wamegundua kuwa ukila fenesi na kunywa bia inaweza kuhatarisha maisha yako na kupelekea kufa.

Ndani ya fenesi kuna chembechembe za sulphur kwa wingi ambazo hupunguza mfumo wa Alidehaidi dehydrogenase kwa asilimia sabini. enzyme hii ni muhimu katika kusafisha sumu ya pombe, kwa wenye ugonjwa wa kisukari hali hii huweza kusababisha mishipa ya damu kuziba au kupasuka, na pengine kusababisha kiharusi."


No comments: