Thursday, January 18, 2018

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akichanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa boma la madarasa ya shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akipiga plasta kwenye chumba cha madarasa katika ujenzi wa shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akitunukiwa uchifu kutoka kwa Machifu wa Kabila la Wasafwa kama shukurani kwa jitihada za kuamsha ari ya wananchi kujitolea kuchangia shughuli za maendeleo katika ujenzi wa shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo jiji la Mbeya Mkoani Mbeya wakati wa ziara ya yake ya kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea kufanya kazi za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akiwa na vazi la kichifu la kabila la Wasafwa pamoja na machifu wengine wa Kabila la Wasafwa wakati alipotunukiwa uchifu wa kabila hilo katika ujenzi wa shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo Jiji la Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi wakishiriki kutekeleza utoaji wa haki ya kumwendeleza Mtoto kwa kumpa elimu.
\
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akikabidhi moja ya mbati 49 kwa uongozi wa Kata ya Mwasanga iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya jamii kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao ili kutoa haki ya Mtoto kuendelezwa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwasanga na maeneo ya jirani katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya na kuhamasisha harambee ya kumalizia ujenzi wa madarasa matatu ya Shule ya Sekondari ya kata iliyozaa kiasi cha shilling laki nane katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kufanya shughuli za maendeleo.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwasanga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile mara baada ya kushiriki kazi yakuchanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Mwasanga iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akitoa mchango wake kwa wazee wa Kata ya Mwasanga iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya kwa ajili kuwawezesha kupata Kadi ya Bima ya Afya kwa Jamii (CHF) katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika ngazi mbalimbali.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW



Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesimikwa rasmi kuwa chifu wa kabila la Wasafwa linalopatikana katika mkoa wa Mbeya .

Dkt. Ndugulile amesimikwa uchifu huo wakati wa ziara yake mkoani Mbeya yenye lengo la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wizara yake imeamua kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi za Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushiriki kwa vitendo kwa kufanya kazi na jamii kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, kilimo, barabara, viwanda na maji, nk.

Ameongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kufuatilia namna ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii ambayo inasisitiza ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli au miradi ya maendeleo ikiwemo upanuzi na uendelezaji wa miundo mbinu mijini na vijijini kama Shule, Barabara, Zahanati na Maghala kwa kutumia rasilimali zilizopo.

“Niwapongeze kwa kazi nzuri mliyofanya na hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii inayotoa matokeo yenye mashiko na tija katika jamii. Tumieni stadi na mbinu shirikishi kuwezesha maendeleo jumuishi ambapo makundi yote katika jamii yanashiriki katika maendeleo yao” alisistiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile pamoja na kupewa uchifu, kushiriki katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Mwasanga pia aliendesha harambee ya kuendeleza ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata hiyo na kuwalipia wazee watano wa Kata hiyo kadi ya kupata huduma za Afya bure kupitia Huduma ya Afya kwa Jamii (CHF).

Kwa upande wake katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya Bw. Hassan Mkwawa amempongeza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) kwa kuamua kushirikiana na wananchi na viongozi kufanya kazi ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kushiriki ujenzi wa shule ya Sekondari ambayo itasaidia watoto kupata haki yao ya kuendelezwa.r

Mmoja ya wananchi wa Kata ya Mwasanga Bw. Fredy Mwaikese ameishukuru Serikali kwa kuunga mkono jitihada zao na kuwashauri wananchi wenzake kuendelea kujitolea kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo na kuchangia shughuli nyingine za maendeleo.

“Ushiriki wa jamii katika kutekeleza kazi na miradi ya maendeleo huharakisha kufikiwa kwa malengo muhimu ambyo ni kipaumbele cha wananchi katika ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla” alisema Bw. Mwaikese.

Wote kwa pamoja tuendelee kushirikiana pamoja kuibua miradi inayozingatia mahitaji ya wananchi kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira yao kwa ajili ya kusukuma mbele maendeleo ya watoto, wanawake na wanaume kwa kuzingatia uzalendo kwanza na kuchapa kazi kwa bidii na kwa kuunga mkono kazi za maendeleo zinazofanya wananchi wa Kata ya Mwasanga kushiriki kwa hali na mali kukamilisha madarasa ya watoto wao kosa fursa ya kuendelea na masomo ya sekondari kwa mwaka 2018. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alichangia mifuko 49 ya saruji na kuendesha harambee kiasi cha shilingi 728,050/= tasilimu kusaidia kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.

No comments: