Saturday, January 20, 2018

DC LYANIVA AWAASA WATAALAMU WA MANUNUZI KUWA WAZALENDO

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewaasa Wanafunzi wanaosoma masuala ya Ununuzi na Ugavi katika chuo cha Uhasibu TIA  Kuwa Wazalendo pindi wanapofika katika maeneo yao ya kazi ili wawe mfano bora kwa Taifa.

Dc Lyaniva ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua mafunzo ya Masuala ya ununuzi na Ugavi,yaliyoandaliwa na Bodi ya PSPTB kwa wanafunzi wa Chuo cha TIA ambao wanasoma masuala ya manunuzi.

"Msiwe na mawazo ya kufikiria kupata pesa za haraka haraka pindi mnapopata kazi,kwani mkiwa na moyo huo mtaangukia katika makosa ya uhujumu Uchumi ,jambo ambalo watu wengi wa taaluma yenu mwisho wa siku wamekuwa wakiangukia Polisi"amesema Dc Lyaniva.

Ameaongeza kwa kusema kuwa anapenda kuwambia kwamba Maadili yenye Uzalendo ndio nguzo ya Msingi  katika kufanya kazi, ndio Maana Rais wetu Dk John Magufuli amefanikiwa kubadilisha mambo mengi katika nchi kutokana na uzalendo wake.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu cha TIA Kampasi ya Dar es Salaam, wanaosoma Masuala ya Manunuzi wakati wa Semina Maalum iliyoandaliwa na bodi ya Wataalam wa Manunuzi PSPTB
 Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Wataalam wa Manunuzi nchini, Godfred Mbanyi akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha uhasibu cha TIA ambao walikuwa wanapata Semina Maalum juu ya masuala ya Manunuzi.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu TIA, Mugisha Kamala akizungumza kwa ajili ya kuwakaribisha wageni na Mkuu wa Wilaya ya Temeke katika Semina hiyo ya masuala ya Ununuzi na Ugavi
 Mwenyekiti wa PSA katika Chuo cha TIA, Baraka Selemani akizungumza kuhusu umuhimu  wa klabu za PSA katika chuo hicho na vyuo vingine vinavyotoa kozi ya Manunuzi
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Nhini(TIA), Furahini Mmbakweni akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi wakati wa Semina hiyo
 Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Bodi ya Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu nchini(TIA) juu ya umuhimu wa wataalamu wa manunuzi kuzingatia maadili pindi wanapokuwa kazini.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akiagana na baadhi ya watendaji na wataalamu wa masuala ya Manunuzi na Ugavi
Sehemu ya Wanafunzi waliohudhuria Mafunzo ya masuala ya Ununuzi na Ugavi kutoka PSPTB yaliyoendeshwa katika Chuo cha uhasibu TIA

No comments: