Tuesday, December 5, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA WADAU WA SEKTA ANAZOZISIMAMIA JIJINI DAR LEO

Pix 3
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akizungumza alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 2
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Pix 1
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi (wapili kushoto) akizungumza wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Mhe. Juliana
Pix 5
Mjumbe wa kamati ya uzalendo Bw. Mrisho Mpoto (kulia) akizungumza wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
Pix 6
Mwanamziki mkongwe nchini Bw. John Kitime (aliyesimama) akichangia wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Pix 7
Baadhi ya wadau wa sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Pix 8
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akimkabidhi mshindi wa shindano la Ubingwa wa Dunia uzito wa kati Bw. Ibrahim Class hundi ya shilingi milioni kumi na nane wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM


Na Shamimu Nyaki – WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania wote kujitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni ya kitaifa ya Uzalendo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 08 Desemba 2017 mjini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Wizara yake imeamua kuanzisha Kampeni ya Uzalendo ili kuwakumbusha watanzania kupenda,kujali na kuthamini nchi yao kwa kuenzi na kuupenda Utamaduni wa Taifa letu ambao ndio unaounganisha na kutambulisha watanzania.
“Uzalendo wetu umetikisika ni lazima sasa kuamka na kujua kuwa tuna jukumu la kuenzi Uzalendo tuliojengewa na Waasisi wa Taifa letu  wa kupenda nchi yetu na kudumisha Utamaduni wetu”Alisema Mhe. Waziri Mwakyembe.
Aidha amewataka watanzania pia kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha katika maisha ya kila siku kwa kuwa Lugha hiyo ndio inayotambulisha Mtanzania popote anapokuwa pamoja na kuheshimu alama zote za Taifa ikiwemo Bendera ambapo ameagiza matumizi sahihi ya Bendera hiyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Juliana Shonza amesema Kampeni hiyo ni muhimu sana kwa Taifa letu kwakua inalenga kukumbusha jamii Utamaduni wetu ambao ndio unafanya jamii kuwa na uzalendo katika nyanja zote za maendeleo.
“Ili kufikia adhma ya Serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda bila kuwa na uzalendo wa kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana.” Alisema Mhe. Juliana.
Mhe. Juliana ameongeza kuwa Wasanii wanahabari na wanamichezo wanajukumu kubwa sana la kuutangaza Kampeni hii lakini pia kuelimisha jamii maana ya Uzalendo pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kutenda mambo mazuri yanayoendana na Utamaduni wa Tanzania kwa wao ni kioo cha jamii.
Naye msanii Mrisho Mpoto ameiahidi Serikali kushirikiana nayo katika kuelimisha jamii maana ya uzalendo kupitia sanaa yake ambapo amesema atashirikiana na wasanii wenzake kuandaa nyimbo zitakazowakumbusha watanzania umuhimu wa Uzalendo ili kuwa na Taifa lenye jamii inayotambua maana ya uzalendo kama ilivyokuwa enzi za mababu zetu.



Kampeni ya uzalendo yenye Kauli mbiu “UZALENDO NA UTAIFA,NCHI YANGU KWANZA” ina lengo la kurejesha hali ya watu kupenda nchi yao  kupinga mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa Umma,kuongezeka kwa tuhuma za rushwa,kuibuka kwa ufisadi,matumizi mabaya ya mamlaka na ubaguzi wa aina yeyote ambapo itakuwa inaadhimishwa kila mwaka.

No comments: