Tuesday, December 12, 2017

Waziri Mahiga awaasa Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Wazalendo na kusimamia maslahi ya Jumuiya

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga(katikati) akiongea katika kikao cha uongozi wa Wizara hiyo na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Disemba 2017. Pembeni yake kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba na kulia ni Mwenyekiti wa Wabunge wateule wa Bunge la Afika Mashariki, Mhe. Abdullah Makame. 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akiongea katika kikao hicho ambapo aliwakaribisha Waheshimiwa Wabunge wateule pamoja na kuwaeleza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ipo tayari kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao. Pembeni yake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi. 
Mwenyekiti wa Wabunge Wateule wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Abdullah Makame akiushukuru uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kikao kizuri cha utangulizi kabla ya kuanza kwa Bunge hilo na pia akaahidi kuwa wataenda kuliwakilisha Taifa vizuri sambamba na kusimamia maslahi ya Jumuiya kwa maendeleo na ustawi wa wananchi wake. 
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge Wateule wa Bunge la Afrika Mashariki wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani) 
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia kikao hicho. 
Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao hicho. Kutoka kulia Bw. Eliabi Chodota, Bw. Bernard Haule na Bw.Joachim Otaru
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Stephen Mbundi akitoa ufafanuzi kuhusiana na taratibu na miongozo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Waheshima Wabunge Wateule. 
Mhe. Waziri na Naibu Waziri wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Picha ya pamoja uongozi wa Wizara na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

1 comment:

BUGDADI AJM BUGDADI said...

Ni vyema ungetaja majina ya watueleweshe waeleweke