Na Rhoda Ezekiel Kigoma.
WAKULIMA wa Sikimu ya Umwagiliaji ya Mpunga Katika vijiji vya Katengera na Ruhiti Wilayani Kakonko, wametakiwa kuongeza ufanisi kwa zao la Mpunga ilikuzalisha mazao ya kutosha kutokana na zao hilo kuwa zao la biashara kwa Wilaya hiyo na serikali kwa kushirikiana na wawekezaji wamewekeza fedha nyingi ilikuinua uchumi wa Wananchi hao.
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, wakati akikabidhi vifaa vya upaliliaji kwa kikundi cha upaliliaji vyenye thamani ya shilini 12,700,000 vilivyo tolewa na shirika LINK vitakavyotumika Kupalilia Katika Mashamba ya Mpunga katika sikimu ya Katengera na Ruhiti lengo ikiwa ni kuwaongezea kipato Wanawake wanaojishughulisha na upaliliaji pamoja na wakulima wa mpunga kwa kuongeza uzalishaji.
Mkuu huyo aliwaagiza wakulima hao kuongeza uzalishaji kutokana na serikali kwa kushirikiana na Wafadhiri wametatua changamoto ya vifaa vya kupalilia vilivyo kuwa vikisababisha kupata mazao machache na kuwataka kulima misimu miwili na kila hekali moja kuzalisha gunia 40 hadi 45 tofauti na kipindi ambacho walikuwa hawana nyenzo hizo.
" niwaombe wakulima wote kulima marambili katika sikimu hii sikimu hii ni ya umwagiliaji kwahiyo maana ya kumwagilia lazima mlime na kiangazi, serikali imeweka fedha nyingi sana katika sikimu hii lazima mjitahidi kuzalisha ilituweze kupata viwanda vya kukoboa mpunga na kuinua uchumi wa wanakakonko kwa yeyote atakae shindwa kulima marambili tutachukua shamba lake na tuwagawie wawekezaji iliwaweze kuwekeza zaidi na kupata mazao ya kutosha", alisema Ndagala.
Hata hivyo Ndagala aliwaagiza Wakulima hao kuzingatia maelekezo ya mabwana shamba katika uwekaji wa mbolea, pamoja na kuzingatia Muda wa kupalilia ilimuweza kuongeza uzalishaji na kupata mazao yenye ubora.
Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya Wafadhiri Mkurugenzi wa Shirika la RERAI shirika linalo shughulika na ongezeko la uzalishaji katika kilimo cha mazao mbali mbali Dr Brigton Gwamagobe, alisema Waliona Wakulima hao wanaahangaika katika upaliliaji na kuomba wafadhiri kuwasaidia kuwapa vifaa na kutoa vifaa 50 vyenye thamani ya milioni kumi na mbili vitakavyo gawiwa katika sikimu ya Katengera na Ruhiti.
Alisema kabla ya vifaa hivyo kutolewa katika vikundi vya upaliliaji hekali moja ilikuwa ikipaliliwa kwa siku moja bei ya kupaliliwa ilikuwa 13,5000 kwa hekali na sasa itakuwa ni hekali 50000 uzalishaji utaongezeka kutokana na wakulima wengi walikuwa wanashindwa kupata mavuno ya kutosha kutokana na kutopalilia kwa wakati na kutumia kemikali kuuwa wadudu lakini kifaa hicho kitumika kuuuwa wadudu pamoja na gharama nafuu za upaliliaji.
Kwa upande wake Katibu wa Kikundi cha upaliliaji Yasinta Mathiasi aliishukuru serikali pamoja na Wawekezaji kwa kuja kuwekeza katika sikimu hiyo na vifaa hivyo vitawasaidia kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na kuepukana na adha ya kuumwa na wadudu waliokuwa wakikaa kwenye maji ya mpunga pamoja na kukatwa na majani.
Alisema kwasasa uzalishaji utaongezeka kutokana na zao hilo likipaliliwa mapema linaongeza uzalishaji kutokana na kupata nafasi ya kukua vizuri na kuepukana na majani yanayozuaia zao hilo kukua kwa Wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabidhi vifaa vya upaliliaji kwa kikundi cha upaliliaji vyenye thamani ya shilini 12,700,000 vilivyo tolewa na shirika LINK vitakavyotumika Kupalilia Katika Mashamba ya Mpunga katika sikimu ya Katengera na Ruhiti lengo ikiwa ni kuwaongezea kipato Wanawake wanaojishughulisha na upaliliaji pamoja na wakulima wa mpunga kwa kuongeza uzalishaji.
No comments:
Post a Comment