Thursday, December 7, 2017

BULEMBO AWATAKA WANA CCM KIGOMA KUWA WAMOJA NA KUHAKIKISHA MAJIMBO YOTE YALIYOKO UPINZANI YANAREJESHWA.

Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, ambae pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma,Abdallah Burembo amewaagiza Viongozi wapya wa Chama hicho Mkoani Kigoma kuhakikisha Wanayarudisha majimbo ya Kigoma mjini na Kakonko na kata zote zilizochukuliwa na upinzani .

Aidha amewataka kufanya kazi ya chama ya kusimamia ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuwatuma kazi Viongozi wa serikali, na kuwakagua kama Wanatekeleza pamoja na kuwaacha Wabunge kufanya wajibu wao na kuacha Makundi makundi katika siasa kwa kuwaweka Wana CCM pamoja ilikuhakikisha ushindi wa majimbo yote kigoma .

Wito huo ameutoa  jana, baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Mkoa katika Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Kumchagua Mwenyekiti wa Mkoa , Mjumbe wa baraza kuu taifa NEC na wajumbe wa halmashauri kuu ya Mkoa, ambapo Burembo aliwapa pole viongozi hao waliochaguliwa kwakuwa Wanakazi kubwa ya kuhakikisha Majimbo yanayotawaliwa na chama tawala yaendelea kuwepo na kuyarudisha yale yote yaliyo chini ya upinzani pamoja na kata zote.

Hata hivyo katika uchaguzi huo nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa ilichukuliwa na Amandusi Nzamba aliewashinda wenzake watano kwa kura 371 akifatiwa na Hamis Betese kura 249 akifuata aliekuwa mwenyekiti wa zamani Amani Kabour 97, Philipo Tabhiliho kura mbili na Antony Mpozemenya tisa,pamoja na nafasi ya Mjumbe wa baraza kuu taifa ilichukuliwa na Kilumbe Ngenda alie shinda kwa kura 426 kati ya Wagombea wenzake Asha Baraka na Atanasi dyoya.

"Tutawapima viongozi mliochaguliwa pamoja na viongozi wa serikali kutokana na ushindi tutakao upata hatuwezi kishindwa katika uchaguzi wakati Dc upo Mkurugenzi Upo na Mkuu wa Mkoa upo, serikali ni ya chama cha mapinduzi waliopo chini ya serikali wanaitumikoa serikali na kutekeleza ilani yetu kama kuna mtendaji au mkurugenzi hafuati utekelezaji wa ilani tutawatoa tuambieni wanao sababisha sisi tushindwe kuaminika hatuwezi kukubari tuyakose majimbo haya tunayataka kwa gharama yoyote ile", alisema Mwenyekiti wa jumuia ya Wazazi.

Alisema WanaCCM jimbo la kigoma mjini wanaiua CCM kutokana na undugu wao, kwenye kushika dora hakuna undugu hawezi kuhama mtu jimbo lilikuwa la CCM alafu wanagawa jimbo kwa upinzani, hili ndio kioo cha Kigoma kuna miradi mingi inatekelezwa ni kwa ilani ya chama cha mapinduzi miradi ya maji,viwanja vya ndege kigoma mjini mnatakiwa kuomba toba maana ni aibu vitu haiwezekani serikali iwaamini alafu Wanachama wawasaliti .

Nae Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Kigoma Amani Kabour alisema Ccm inamafanikio Makubwa kwa Mkoa wa Kigoma wanazungumza wakati akiachia madaraka wakiwa na mawaziri watatu na naibu waziri wa kigoma CCM ni chama cha mfano tofauti na kipindi cha nyuma na kigoma imekuwa ni Mkoa waliochagua wabunge wawili na wengi ni wapya pamoja na wabunge sita wa kuchaguliwa na Wawili viti maalumu hivyo viongozi waliochaguliwa kihakikisha majimbo yaliyo chini ya upinzani wanayarudisha.

Aidha aliwaomba viongozi waliochaguliwa kuhakikisha Wanapambana na ufisadi ,uzembe pamoja na kukemea rushwa ilikuhakikisha mkoa wa kigoma unasonga mbele na kuondokana na dhana ya kwamba mkoa huo ni mkoa wa mwisho kwa umasikini ilikuhakikisha Wananchi wanakiamini chama na kuendelea kutoa ushirikiano.

wako tayari kufanya uchaguzi waweze kupata viongozi watakao saidia kuipelwka CCm mbele kuhakikisha CCM ni chamaa kinachotawala Mkoa wa Kigoma na kuo mkoa wa maendelea ubadhilifu na ufisadi na ujambazi kuwaomba kama viongozi wakui kusimamia na kuhakikisha Mkoa unaondokana na rushwa na ufisadi katika

No comments: