NA K-VIS
BLOG, FELIX ANDREW
WAAJIRI Tanzania Bara wametakiwa kuwashirikisha
wafanyakazi wao kabla ya kufanya maamuzi mbali
mbali ili kuendelea kudumisha amani na mshikamano maeneo ya kazi.
Ushauri huo ulitolewa jjini
Dar es Salaam jana na Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira na Vijana , Anthony Mavunde, wakati akizindua baraza
la wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC)
Alisema kuwa uongozi
shirikishi na wa pamoja ndiyo njia pekee itakayopunguza migogoro maeneo ya
kazi, hivyo waajiri hawana budi kuhakikisha jambo hilo linazingatiwa ipasavyo.
“Lengo kuu la
uongozi shirikishi na wa pamoja ni kujadiliana changamoto mbali
mbali na kuzitatua kwa nia ya kufikia malengo,” alisema.
Mavunde aliwaasa wafanyakazi
nchini kuondokana na urasimu katika kutoa huduma mbali mbali kwa
jamii.
“Urasimu katika utoaji wa
huduma ni changamoto kubwa sana ambayo inaisumbua nchi naomba sana
msifanye hivyo kwa manufaa ya taifa letu,” alisema.
Aidha naibu waziri huyo
alisisitiza kwa waajiri wasio jiunga na Mfuko huo kufanya hivyo mara moja kabla
sheria haijachukua mkondo wake
Alisema kuwa serikali
itaanzisha msako mkali mwakani wenye lengo la kuwakamata na kuwafikisha kwenye
vyombo vya sheria waajiri wote ambao bado hawajajisajili na mfuko huo.
Aliongeza kuwa serikali
ilikwisha toa muda wa kujisajili kwa wasiofanya hivyo ambao ulimalizika tarehe
30 Septemba mwaka huu.
Mnamo mwezi Januari mwakani
tutaanzisha msako wa kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola waajiri
wote ambao wameshindwa kujisajili na mfuko hadi sasa, alisema
Kwa mujibu wa sheria ya fidia
kwa wafanyakazi namba 263 waajiri wote wanatakiwa kujisajili na mfuko
Sheria inawataka waajiri
katika sekta ya umma na binafsi ambao wana zaidi ya mfanyakazi mmoja
kujisajili na mfuko.
Kifungu cha 71( 4) cha sheria
kinasema kushindwa kujisajili na mfuko ni kosa na endapo itathibitika mwajiri
anaweza kutozwa faini isiyozidi kiasi cha shilingi milioni kumi au kifungo cha
miaka mitano gerezani.
Kuhusu baraza, alisema kuwa
ni muhimu kwa maendeleo na kuwataka wafanyakazi nchini kuyatumia kwa
lengo la kupunguza msuguano sehemu za kazi.
“Waaajiri na wafanyakazi
wanatakiwa kutumia baraza hili kwa kuleta amani na kuimarisha utendaji kwa
maendeleo ya nchi yetu,” alisema.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la WCF Bw Masha Mshomba, alisema
kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuwashirikisha wafanyakazi katika maamuzi mbali
mbali ya kiutendaji tayari menejimenti kwa kushirikiana na tawi la
chama cha wafanyakazi wa serikali na afya (TUGHE) imekamilisha
uundaji wa baraza hilo.
Aliongeza kwa mfuko huo
umeendelea kutimiza majukumu yake katika kuchangia maendeleo ya
taifa , husani uchumi wa viwanda kwa kuendelea kuwahudumia wafanyakazi wanoumia
au kuugua kutokana na kazi kwa nia ya kuwawezesha kurudi kazini.
Aidha mfuko pia unashiriki
moja kwa moja katika kujenga uchumi wa viwanda kwa njia ya ubia na
Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii nchini.
Katika kusogeza huduma jirani
na wadau wote , alisema mfuko umepanga kufungua ofisi zake katika mikoa minne
katika robo ya tatu ya mwaka 2017/18
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni
Dodoma, Arusha , Mwanza na Mbeya huku lengo likiwa ni kuwa na ofisi katika
mikoa ishirini.
Hadi mwishoni mwa mwezi
Novemba mwaka huu mfuko huo ulioanzishwa mwaka 2015 ulikuwa umesajali zaidi ya
waajiri 12,000 na kulipa fidia kwa zaidi ya wafanyakazi 280
walioumia na kufariki kutokana na ajali za mahali pa kazi.
Mhe. Mavunde
akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi huo.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba. Kulia mni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la WCF, Bi. Amina Likwangala.
Mhe. Mavunde akizungumza na waandishi wa habari.
Bw.Mshomba akizungumza na waandishi wa habari.
Picha ya pamoja
Bw.Masha akizungumza kabla ya uzinduzi huo
Mhe. Mavunde, (katikati), Bw. Masha Mshomba (kushoto) na Bi Amina Likwangala wakifurahia jambo. |
Mhe. Mavunde, (wapili kushoto) na Bw. Masha Mshomba, (wakwanza kushoto), wakiungana na wafanyakazi kuimba wimbo wa mshikamano.
Mhe. Mavunde akiongozana na Bw. Mshomba
Mhe. Mavunde akipokea Mkataba wa kuunda baraza hilo kati ya uongozi wa WCF na chama cha wafanyakazi TUGHE, tawi la WCF, kutoka kwa Katibu wa Baraz hilo, Bw.Geofrey Masisa.
Wafanyakazi wa WCF wakiimba wimbo wa mshikamano.
Baadhi ya wafanyakazi wa WCF waliohudhuria hafla hiyo.
Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Anthony Mavunde (wapili toka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba (wa kwanza kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza la kwanza la Wafanyakazi wa Mfuko mapema leo Desemba 22, 2017 jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la WCF, Bi. Amina Likwangala. Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Masha Mshomba (kulia) wakionyesha
Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WFC) wakifurahia uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment