Na Mathias Canal, Mtwara
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) ambayo Kitaifa inaratibu Utafiti wa zao la Korosho, Mbegu za mafuta na mazao jamii ya mizizi (Muhogo na viazi vitamu) Dkt Omari Mponda ameagizwa kuwaongeza malipo ya kazi wafanyakazi wa kituo hicho katika mradi wa kubangua Korosho.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo 22 Disemba 2017 wakati akizungumza na wafanyakazi wa kituo hicho cha Utafiti Mara baada ya kutembelea kiwanda kidogo cha kubangua Korosho na kubaini kuwa wafanyakazi hao wanalipwa shilingi 600 kwa kila kilo moja ya korosho wanayobangua kiasi ambacho hakiakisi ufanisi wa kazi kubwa wanayoifanya.
Katika maelekezo yake Naibu Waziri huyo amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho kuongeza kiasi cha malipo walau kufikia shilingi 1000 kwa kila kilo moja wanayobangua ili wafanyakazi hao waweze kupata malipo ambayo yatamudu gharama za maisha.
Sambamba na hayo pia ameupongeza Uongozi wa kiwanda hicho kwa kubuni ajira hizo mpya za mradi huo wa korosho zinazowanufaisha wananchi wa Mtwara sambamba na pongezi za kuajiri wafanyakazi wengi ambao asilimia kubwa ni wanawake.
Aidha, amesisitiza kuongeza bidii ya utoaji Elimu kwa wananchi kufahamu umuhimu wa mazao ya muhogo, Njugu na Mbaazi ili yaweze kutumika zaidi kwani ni fahari kwa wakulima na wananchi kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Mhe Mwanjelwa ameipongeza Taasisi hiyo kwa kufanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kutoa/kugundua na kusajili mbegu bora 54 za korosho kwa ajili ya matumizi kwa wakulima mwaka 2006 (Aina 16), Mwaka 2015 (Aina 22 mbegu chotara), na Mwaka 2016 (Aina 16 mbegu fupi).
Alisema Aina hizo za mbegu hizo zina uwezo wa kuzaa korosho nyingi na bora, Zina uwezo wa kuvumilia magonjwa na wadudu waharibifu na kufanya Utafiti kupendekeza zaidi ya Aina 30 za viuatilifu vya kudhibiti visumbufu vya Korosho.
Taasisi ya Utafiti wa kilimo Naliendele (NARI) imepewa jukumu la kufanya Utafiti ili kuongeza tija katika Kilimo katika kanda ya kusini mikoa ya Lindi, Mtwara na Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua miche ya Korosho wakati alipotembelea Kitalu Nyumba (Green House) katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) Mkoani Mtwara Mwingine ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) Dkt Omari Mponda, leo 22 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Tanki linalohifadhi maji kwa ajili ya Skimu ya umwagiliaji wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) Mkoani Mtwara, leo 22 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akishiriki kazi ya kubangua korosho wakati alipotembelea Kiwanda cha Korosho na Juice katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwara, leo 22 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua shamba lenye mfumo wa kisasa wa umwagiliaji kwa Skimu ya umwagiliaji wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) Mkoani Mtwara, leo 22 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akishiriki kazi ya kubangua korosho wakati alipotembelea Kiwanda cha Korosho na Juice katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwara, leo 22 Disemba 2017.
No comments:
Post a Comment