Saturday, December 9, 2017

HUDUMA YA USAFIRI WA APP YA TAXIFY YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

Taxify, App ya huduma ya usafiri inayokuwa kwa kasi barani Ulaya na Afrika, leo imezinduliwa jijini Dar es Salaaam, huku mamia ya madereva wakiwa wamejiorodhesha ili kutoa huduma katika sehemu mbalimbali za jiji.

Katika kusherehekea uzinduzi wa huduma hiyo mpya, Taxify imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo kwa fedha ya Shilingi ya Kitanzania; Sh 600, Sh300 kwa kila kilometa moja. Sh 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000.

“Dar es Salaam ni jiji lenye soko kubwa na lenye faida kwa usafiri wa watu binafsi mijini na sehemu muhimu ya shughuli za kibiashara ambapo shida kubwa ya kutumia usafiri binafsi maeneo ya mjini hutokea.

Tunayofuraha kubwa kuzindua huduma hii hapa na tuna uhakika Taxify itasaidia kwa kiasi kikubwa kuchangia kwa ufanisi katika ushindani wenye afya na kuboresha ubora wa huduma huku tukitoa kutoa fursa kwa madereva kujipatia kipato kizuri,” alisema Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Kanda, Taxify.

Taxify inachukua asilimia 15 pekee ya mapato kutoka kwa madereva wake, ikiwa ni gharama ndogo zaidi ukilinganisha na washindani wetu wa kibiashara wanaochokua asilimia 25. Kamisheni ndogo ambayo inachukuliwa na Taxify inatufanya tuweze kupunguza gharama ya huduma kwa wateja wetu na kuhakikisha madereva wanapata kipato cha kukidhi mahitaji ya familia.

Furaha ya madereva humaanisha huduma nzuri na bora kwa watumiaji wa usafiri wetu. Taxify inaamini katika kuheshimiana na madereva wake na kuhakikisha wanapata zaidi ya kile wanachopata kwenye mitandao mingine huku ikiwapa aina mbalimbali za ulinzi na vipengele vinavyowasaidia kufanya kazi kwa njia inayofaa kwao. 

Pia kampuni hii inaamini katika kutoa huduma bora kwa wateja wanaotumia usafiri huu pamoja na msaada wa karibuni kutoka kwa timu yetu ikiwa ni pamoja na kuwapa chaguo la kulipia huduma kwa pesa taslimu.

Taxify tayari inatoa huduma zake kwenye nchi 20 duniani na imeonyesha mafanikio makubwa kutokana na huduma zake nafuu na uwazi katika uendeshaji.

Taxify pia inapatikana kwenye mfumo wa IOS na Android.
 Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify Kanda ya Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa App hiyo leo jijini Dar es salaam. Taxify ni App inayotoa huduma ya Usafiri ambayo inakuwa kwa kasi barani Ulaya na Afrika. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka. 
 Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify Afrika Mashariki (kulia) na Remmy Eseka, Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania wakibonyeza vitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya Taxify leo jijini Dar es salaam. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000.
 Nyota wa filamu za bongo, Wema Sepetu (katikati) akijumuika pamoja na Meneja Masoko wa Taxify Afrika Mashariki, Lorreen Ajiambo (kulia) na Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini Tanzania, Remmy Eseka kuzindua App mpya ya Taxify inayotoa huduma ya usafiri leo jijini Dar es salaam. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000. 
(Kutokea kushoto) Maafisa wa Taxify, Shivachi Muleji Meneja Maendeleo wa Taxify Kanda ya Afrika Mashariki, Remmy Eseka Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini Tanzania na Meneja Masoko wa Taxify Afrika Mashariki, Lorreen Ajiambo kwa pamoja wakimuonyesha Nyota wa filamu za kibongo Wema Sepetu jinsi App hiyo inavyofanya kazi katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000.

No comments: