Sunday, December 3, 2017

DK. KIGWANGALLA AAGIZA NDANI YA SIKU 30 KUJITOKEZA WAMILIKI WA MAGOGO YALIKAMATWA BANDARINI DAR

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ametoa muda wa siku 30 kwa wahusika ambao ni wamiliki wa magogo yaliyokamatwa katika bandari ya Dar e s Salaam (TPA) ambayo yalikuwa yasafirishwe nje ya Nchi, kujitokeza haraka kueleza wameyato wapi na walikuwa na lengo gani baada ya kuyatelekeza bandarini hapo kwa muda wa miaka 10 sasa huku mengine yakitelekezwa pasipo kuwa na vibali maalum.

Dk.Kigwangalla ametoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini hapo kukagua mali na bidhaa zinazoshughulikiwa na Wizara yake hiyo ambapo katika zkukagua kwake huko alibaini uwepo wa makontena hayo 55 ambayo yapo kwa miaka 10 sasa yakihifadhiwa huku wahusika wakishindwa kujitokeza.

“Naagiza mamlaka zilizo chini ya wizara yangu kuhakikisha wanahakiki magogo yote yalipo hapa bandarini. Mwenye huu mzigo lazima ajulikane hasa haya magogo 938, Ndani ya siku 30 mwenye haya magogo atangaziwe na ajitokeze vinginevyo itabaki kuwa mali ya Serikali” alisema Dk. Kigwangalla.

Hata hivyo aliagiza pia kontena 55 zilizokutwa bandarini hapo zenye magogo pia nazo wahusika wajitokeze na nyaraka zao kamili ili waeleze kama kweli wameyatoa Zambia magogo hayo ama sehemu gani hivyo wajitokeze na wasipofanya hivyo ndani ya siku hizo 30, magogo hayo yatataifishwa na kuwa mali ya Serikali.

Katika ziara hiyo, Waziri Dk.Kigwangalla aliweza kutembelea bandari ya Dar es Salaam pamoja na maeneo yanayohifadhiwa magogo hayo zikiwemo bandatri ya nchi kavu ya NASACO, Malawi (Malawi Cargo) na baadae eneo hilo la bandari ya Dar es Salaam.

Akiwa katika eneo la Malawi Cargo, Waziri Dk. Kigwangalla aliweza kushuhudia makontena mbalimbali yakiwemo yale ya mbao aina ya mitiki ambayo inatarajiwa kusafirishwa nje ya nchi huku akibaini uwepo mkubwa wa udanganyifu kwa wasimamizi wa upakuaji na usafirishaji katika eneo hilo la bandari ambao awali walitaja idadi ndogo ya makontena ya mbao mbele ya Waziri hali iliyopelekea kuanza kuyakagua makontena yote ndani ya eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangallaakitoa maagizo kwa uongozi wa bandari ya TPA.
Baadhi ya magogo hayo yaliyokutwa katika makontena bandarini hapo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakiwa katika eneo la bandari ya nchi kavu ya Malawi Cargo. wakati wa kukagua magogo hayo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa nyaraka ya idadi ya makontena katika eneo la Malawi Cargo
Zoezi la ukaguaji likiendelea
Baadhi ya magogo yaliyokutwa bandarini hapo

No comments: