Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi (kushoto), kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume
ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akimkabidhi mbegu ya viazi
lishe kwa ajili ya shamba darasa la Kijiji cha Kibehe, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani Chato leo.
Wanakikundi cha Umoja cha Kijiji cha Kibehe kilichopo Kata ya Kigongo wakiandaa shamba lao la mbegu.
Wanakikundi
cha Umoja cha Kijiji cha Kibehe kilichopo Kata ya Kigongo wakiwa kwenye
uzinduzi wa shamba darasa la viazi lishe na mihogo.
Mtafiti
wa Mazao ya Mizizi wa Wilaya ya Chato, Monica Mulongo akizungumzia
vitamini A inayopatikana kwenye viazi lishe ambayo ni muhimu kwa watoto.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya viazi lishe. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari.
Mtafiti , Ismail Ngolinda
kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro
akizungumzia ubora wa mbegu ya Wema pamoja na upandaji wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari , akionesha mbegu ya mahindi ya Wema baada ya kukabidhiwa. |
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha Maruku mkoani Kagera,
Jojianas Kibula, akiwaonesha wakulima wa Kibehe jinsi ya kupanda mbegu
ya mhogo.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipandikilo, Clara Fidelis akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha Maruku mkoani Kagera,
Jojianas Kibula akitoa maelezo kwa wakulima wa vijiji vya Ipandikilo na
Kitongoji cha Kaseni jinsi ya kupanda mbegu ya mhogo.
Watafiti
Bestina Daniel na Ismail kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga
wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mahindi
katika Kijiji cha Bukiliguru.
Mshauri
wa Jukwaa la ioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus
Nyange akipanda mbegu ya mhogo katika shamba darasa la Kijiji cha Itale.
Wakulima wa Kijiji cha Bukiliguru wakishiriki kuapanda mbegu za mahindi katika shamba darasa.
Mtafiti , Ismail Ngolinda
kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro
akiwaelekeza wakulima jinsi ya kupanda mbegu bora ya mahindi ya Wema
inayovumilia ukame.
Wakulima wa Kijiji cha Bukiliguru wakifuatilia uzinduzi wa shamba la mihogo.
Na Dotto Mwaibale, Chato
WAKULIMA
Wilaya Chato mkoani Geita wamefurahia mbegu bora ya mihogo, mahindi na
viazi lishe waliopewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) ili kuanzisha mashamba darasa ya mbegu hizo na kuzisambaza kwa
wakulima wengine katika maeneo mengine.
Wakizungumza
wilayani hapa leo kwa nyakati tofauti wakati wa uzinduzi wa mashamba
darasa ya mbegu hizo katika vijiji vya Kibehe, Ipandikilo, Kitongoji cha
Kaseni, Kijiji cha Itale na Bukiliguru kilichopo Kata ya Bwanga
walisema mbegu hizo walizokabidhiwa na COSTECH kwa kushirikiana na
Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo ni mkombozi kwao.
Ofisa
Kilimo wa Kata ya Kachwamba, Hamisi Matesi alisema Costech
kuwapelekea wakulima mbegu hizo itawasaidia sana kupata chakula wananchi
wa kata hiyo ziada watauza.
Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Ipandikilo, Clara Fidelis akizungumza kwa niaba
ya wananchi wa kijiji hicho alisema wakulima walikuwa wakipata mavuno
machache ya mahindi na mihogo kwa kuwa hawakuwa na mbegu bora hivyo
baada ya kufunguliwa kwa shamba darasa la mbegu hizo katika maeneo yao
wanategemea kupata mazao mengi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari aliwataka
wananchi hao kutambua kuwa mpango huo wa serikali ya awamu ya tano
unawategemea sana wakulima katika kilimo hivyo fursa hiyo walioipata ya
kupelekewa mbegu hizo wasiipoteze.
“Hakikisheni
mbegu hizi bora za mihogo mnazopewa mnazitunza ili kutoa nafasi kwa
wananchi wengi zaidi kujifunza mbinu bora za kilimo hiki kupitia shamba
darasa hili ili kila mkazi wa Chato aweze kulima na kuzalisha kwa tija”
alisema Mhandisi Hari.
Hari
ameishukuru COSTECH kwa kuamua kuipatia wilaya hiyo mashamba darasa
katika vijiji hivyo kwani anaamini mbegu hizo zitasimamiwa vizuri na
kisha kuwafikia wakulima wengi zaidi ili waweze kuachana na mbegu zao za
zamani ambazo zinashambuliwa na magonjwa ya batobato na michirizi ya
kahawia.
Akizungumza
kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu
hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH,
Dk.Bakari Msangi alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali
katika masuala yote yanayohusu Sayansi na Teknolojia na kusimamia
tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na
kuhakikisha matunda ya tafiti hizo yanawafikia walengwa.
Alisema
mbegu hizo walizozikabidhi ikiwamo ya mahindi yanayostahimili ukame ya
Wema 2109 zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na
baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya
kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu
ambazo zilikuwa na magonjwa kama batobato katika mihogo.
Dk. Bakari aliwataka wakulima hao kuyatunza mashamba darasa hayo na kubwa baada ya muda mfupi watarudi kuangalia maendeleo yake.
No comments:
Post a Comment