Wednesday, November 15, 2017

RC LUHUMBI ASISITIZA WANANCHI KUTUMIA RASILIMALI WALIZONAZO KUCHOCHEA MAENDELEO

Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kuchanganya mchanga kwenye shughuli ya ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Kazibizyo wakati wa zoezi la uhamasishaji wananchi kujitolea katika uchangiaji wa maendeleo ya ujenzi wa zahanati,vituo vya afya na shule Wilayani Bukombe. 
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ambaye yupo (Katikakati)Josephat Maganga akishirikiana na wananchi pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kufanya shughuli ya kuchanganya mchanga. 
Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga msingi wa kujenga zahanati ya kijiji cha Kazibizyo Wilayani Bukombe pamoja na wananchi ambao wamejitokeza kuunga jitihada za serikali za kuleta maendeleo ya huduma za afya maeneo ambayo yanauwitaji . 
Katibu tawala wa wilaya ya Bukombe akishiriki zoezi la ujenzi. 
Wananchi wa kijiji cha Kazibizyo wakishiriki kusomba mawe. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiendelea na harakati za kushiriki ujenzi wa zahanati kijijini hapo. 
Wakina mama wakishiriki zoezi la ujenzi wa zahanati kijiji cha Kazibizyo 
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Josephat Maganga akizungumza na wananchi wa kijiji hicho juu ya kujitolea kwenye swala la maendeleo bila ya kutegemea serikali. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kazibizyo baada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa zahanati kijijini hapo.



NA JOEL MADUKA, GEITA

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wakazi wa kijiji cha Kazibizyo na Bulama kutumia rasilimali walizonazo ili kuchochea maendeleo ya vijiji vyao.

Mhandisi Luhumbi aliyasema hayo katika uzinduzi wa ujenzi wa zahanati kwenye Kata ya Nga’nzo na Shule kwenye kijiji cha Bulama ili kuwaondolea wananchi tatizo la kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.Alisema matatizo mengi yanasababishwa na baadhi ya viongozi kutowajibika badala yake kuweka mbele maslahi binafsi.

“Shida kubwa wananchi tumefanya makosa mengi mno tumekuwa na viongozi bora viongozi sio viongozi bora viongozi ambao awawezi kuamasisha viongozi ambao kazi yao ni kula michango ya wananchi viongozi ambao fedha zikija wanaangalia kupiga kwanza hela ndio wanaleta yale makombo ambayo yanajenga vitu vibovu vibovu,Sasa viongozi wa namna hiyo hatuwezi kuwavumilia Geita,ni bora wafungashe virago watafute Mikoa mingine,kipindi hiki ni kipindi cha kazi kama unaona kazi ni ngumu achia bodi”Alisisitiza Luhumbi.

Mhandisi Luhumbi alisema wananchi ndio nguzo kubwa ya maendeleo kwenye maeneo yao hivyo lazima wawe na afya bora na elimu ili wafanya kazi za maendeleo.Mmoja wa wananchi Bi Sophia Sangizo alielezea wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya na kusababisha wanawake wengi kujifungulia nyumbani hali ambayo imekuwa ikisababisha matatizo kwao.

Naye ,Mzee Mayoke Ambrose Maziku ambaye ametoa kiwanja kwaajili ya ujenzi wa zahanati kijijini hapo alisema kuwa msukumo mkubwa ambao umepelekea kutoa kiwanja ni kutokana na mwaka 2013 na 2007 alipoteza watoto wake kutokana na kukumbwa na umauti sababu kubwa ikiwa ni kuwa mbali na huduma za afya kwani wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita 20 kufuata huduma hiyo.

No comments: