Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kamati ya Fedha na Utawala katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ,imefanikiwa kutekeleza asilimia 98 ya miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokusudiwa kutekeleza katika awamu ya kwanza ya mwaka fedha wa 2017/2018 katika kipindi cha mwezi Septemba hadi Oktoba kutumia Sh bilioni 1.2 kati ya Sh bilioni 2.5 zilizotakiwa kutumika.
Hayo yamesemwa leo na Mchumi wa manispaa hiyo Ando Mwankuga baada ya kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kujionea kile walichopanga, kuwa kimetekelezwa kwa ufanisi, na baadhi ya miradi imekamilika na mingine ikiendelea kutekelezwa kikamilifu.
Amesema katika utekelezaji wa miradi hiyo, kuna changamoto mbalimbali ambapo miradi mingi inaanzishwa lakini haikamiliki kwa wakati,miradi hiyo hufanyika kutokana na vyanzo mbali mbali vya fedha za ndani na ruzuku ya serikali na kukuta mradi ni mkubwa kuliko kiwango cha fedha,kilichopo,pia amewaomba madiwani kupitisha bajeti kulingana na miradi ili kutatua changamoto ya miradi kutofanikiwa.
Aidha amewashukuru madiwani katika manispaa ya ilala kwani ni watu makini na wanaelewa kile wanachokifanya na pia wanakosoa na kutoa changamoto vizuri kwa lengo la kuleta maendeleo katika mispaa hiyo
Miradi iliyokaguliwa ni Ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mvuleni kata ya Msongola, Ujenzi wa Barabara ya Segerea hadi Bonyokwa, Ujenzi wa Kisima na Miundombinu ya maji Mtaa wa Segerea pamoja na Jengo la DMP liliopo ndani ya maanispaa hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni NaibuMeya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amesema kuwa wataalamu waliokabidhiwa miradi wamefanya kazi kwa kuzingatia maadili na uadilifu na kuchangia kukamilika kwake.
Naye Diwani wa Kata ya Segerea, Edwin Mwakatobe amesema miradi iliyotekelezwa kwenye kata hiyo imetokana na fedha zilizotengwa na kutumika ipasavyo.
Afisa Mtendaji Kata ya Msongola Enock Segesela, ameishukuru Manispaa kwa kujenga Ofisi ya Serikali za Mtaa ya Mvuleni kwani awali walikuwa wamepanga katika fremu na kulipa kodi.
Mchumi wa manispaa ya ilala (katikati) Ando Mwankunga akizungumza walipofanya ziara katika ujenzi ofisi ya kata Mvuleni ambapo inaendelea kujengwa.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Enock Segesela,(kulia) akielezea jambo.
Hii ndiyo ofisi ya kata ya Mvuleni inayoendelea kujengwa, ambapo ina chumba cha Mwenyekiti,ofisi ya chumba cha mtendaji kata,ukumbi wa mikutano,choo,pamoja na stoo ya kuifadhi vitu.
Naibu Meya katika Manispaa ya ilala (kushoto) Omary Kumbilamoto pamoja na diwani wa kata ya segerea Edwin Mwakatobe wakikagua Kisima cha maji katika kata ya segerea
Diwani wa kata ya Segerea kushoto akielezea kuhusu mradi wa maji unavyotekeleza na umekaribia kukamilika.
Hapa ni katika daraja la Segerea ambapo diwani wa kata hiyo akielezea changamoto zinazotokea wakati mvua inanyesha ambapo wakazi wa maeneo hata wanakumbwa na adha ya maji kujaa na kuingia katika makazi yao.
No comments:
Post a Comment