Thursday, November 16, 2017

MAHAFALI DUCE YAFANA, PROF MUKANDALA AWAAGA RASMI WANA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewatunukia wahitimu 1443 wa ngazi mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Elimu Dar es salaam (DUCE) kwenye mahafali ya 10 yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

Katika mahafali hayo Mkuu wa Chuo Dkt Kikwete aliwatunukia wahitimu hao sambamba na kutoa zawadi kwa wanafunzi nane waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.

Rais wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam, Prof William Anangiyse amesema kuwa jumla ya wahitimu 1371 wametunukiwa digrii za awali katika fani mbalimbali na Wahitimu 72 ni wa ngazi ya stashahada ya uzamili katika elimu  (PGDE) na kutimiza idadi ya 1443.

Prof Anangisye amesema kuwa jumla ya 928 ni wanaume na 515 ni wanawake huku wahitimu 1015 wakitunukiwa digrii ya elimu ya jamii na ualimu (B.A.Ed), , 233 ni wahitimu wa Sayansi na Ualimu ( B.Sc.Ed), wahitimu 72 ni Elimu katika sayansi (B.Ed.Science) na Elimu katika elimu ya Jamii ( B.Ed.Arts) ni wahitimu 51.
Mbali na hilo, Mwenyekiti wa bodi ya Usimamizi ya Chuo Kikuu Kishirikishi  Cha Elimu Dar es Saalam, Prof. Rwekaza Mukandala kwenye mahafali ya 10 ya chuo hicho amewaaga rasmi wanajumuiya wa Chuo Kikuu Kishirikishi  baada ya kumaliza muda wake wa mwaka mmoja alioongezewa na Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli kwenhe mahafali ya mwaka jana.

Mkuu wa Chuo Dkt Kikwete aliweza kutoa zawadi kwa wahitimu nane waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho pamoja na Emanuel Safari Dadi aliyefanya vizuri kwa ujumla na kumpongeza kwa juhudi kubwa alizozifanya katika kipindi chake cha masomo.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepiga picha na mhitimu Emanuel Safari Dadi aliyefanya vizuri katika mitihani yake yote na kupata GPA 5.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu  Dar es Salaam Peter Ngumbulu (Kulia), Rais wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam Prof William Anangyse, Mlau wa Chuo Kikuu Kishirikishi Cha Elimu Dar es Salaam Prof. Martha Qorro na wajumbe wengine katika mahafali ya 10 yaliyofanyika jana Jijini Dar es salaam.
 Wahitimu wakitoa kiapo cha utii na ahadi katika kulitumikia taifa na kulikuza
 Mhitimu bora Emanuel Safari Dadi akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya wahitimu wote.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa zawadi kwa wahitimu nane waliofanya vizuri kwenye mitihani yao. Chini akiwa amepiga nao picha ya pamoja.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunukia wahitimu wa ngazi mbalimbali katika mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika jana Jijinj Dar es Salaam.


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa mahafali akiongozana na viongozi wengine wa Chuo Kikuu kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam jana katika mahafali ya 10.

No comments: