Shule ya Sekondari Kom iliyopo mjini Shinyanga leo Jumamosi Novemba 11,2017 imefanya mahafali ya 9 ya kidato cha nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2006.
Mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya kidato cha nne mwaka 2017 yaliyohudhuriwa na wazazi na wageni mbalimbali alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.
Akizungumza katika mahafali hayo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema mabadiliko yoyote yanaletwa na ushirikiano hivyo kupitia ushirikiano.lisema shule hiyo imekuwa maarufu nchini kutokana na elimu bora inayotoa na kutokana na hali hiyo imeupatia sifa mkoa wa Shinyanga.
“Sisi kama serikali tunajivunia uwepo wa shule hii katika mazingira yetu kwani inatutangaza, tupo tayari kushirikiana nanyi katika kutatua changamoto zinazojitokeza ili kusukuma gurudumu la maendeleo”,alieleza Matiro.“Tupo tayari kuhakikisha kuwa tunashirikiana na sekta binafsi na milango yetu ipo wazi na panapotokea changamoto msisite kutufikia”,alisema.
Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wazazi kuwekeza kwenye elimu kwa watoto kwani huo ndiyo urithi wenye thamani katika maisha yao.Katika hatua nyingine aliipongeza shule hiyo kuajiri watu 63 katika shule kwani wanaunga mkono lengo la serikali la kuzalisha ajira kwa wananchi.
Aidha aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuanzisha shule ya awali na msingi kitendo ambacho kinatokana na ushirikiano uliopo kati ya shule na wazazi ambao wamekuwa mstari wa mbele kusukuma maendeleo ya shule.
Matiro aliwataka wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kuwa mfano katika maeneo wanakokwenda na kuhakikisha matendo yao yanaendana na mambo waliyofundishwa shuleni.Naye Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari Jackton Koyi aliishukuru serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiwapa katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inafikia malengo yake.
Alisema Kom sekondari shule hiyo imetimiza miaka 12 tangu kuanzishwa kwake na imekuwa daraja la elimu kwa wanafunzi ambao wengi wamekuwa wakiingia kidato cha tano na kujiunga katika vyuo mbalimbali.“Shule yetu imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani,mfano kati ya wanafunzi 160 waliomaliza kidato cha nne mwaka 2015,145 walijiunga na masomo ya kidato cha tano,na mwaka 2016 kati ya wanafunzi 144 waliofanya mtihani wa kidato cha nne,133 walijiunga kidato cha tano”,aliongeza Koyi.
“Naomba wazazi muendelee kutuamini na kuleta wanafunzi katika shule hii ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani mbalimbali”,alieleza Koyi.Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo,Mwita Warioba alisema shule hiyo hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 542,walimu 32 huku akisisitiza kuwa lengo la shule hiyo ni kutoa elimu bora na tayari shule hiyo pia imeanzisha shule ya awali na msingi.“Shule yetu ina miundo mbinu ya kutosha,madarasa yapo ya kutosha,tuna umeme wa Tanesco,maji kutoka ziwa Victoria,mabweni 8,viwanja vya michezo,maktaba moja,maabara mbili ikiwemo ya Computer”,aliongeza Waryoba.
Awali akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne,Jackline Benson alisema walianza kidato cha kwanza wakiwa 104,ambapo wavulana walikuwa 52 na wasichana 52 lakini idadi iliongezeka na hivyo idadi ya waliohitimu kidato cha nne mwaka huu ni 154,kati yao wasichana ni 73 na wavulana 81.
Wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2017 katika shule ya sekondari Kom wakimpokea mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya shule hiyo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa shule ya sekondari Kom,Jackton Koyi akimpokea mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa ajili ya kushiriki mahafali ya kidato cha nne katika shule hiyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwapungia mkono wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kom .
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya mkurugenzi wa shule ya sekondari Kom .
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Zena Ali akimweleza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro historia ya shule ya sekondari Kom wakati wa maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika shule hiyo
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kom wakionesha ramani ya dunia kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati wa maonesho ya taaluma wakati wa mahafali hayo
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Rajuu Masudi ambaye ni mtaalamu wa kuchora akieleza kuhusu sanaa ya uchoraji inayofanywa na wanafunzi wa shule ya sekondari Kom
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kom,Safia Ali akitoa maelezo kuhusu maonesho ya sayansi kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wahitimu wa kidato cha nne 2017 katika shule ya sekondari Kom wakiandamana
Wahitimu wakiandamana kuelekea ukumbini
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikata utepe wakati wa mahafali ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kom.Kulia ni mwenyekiti wa bodi ya shule Peter Kugulu,kushoto ni mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi
Wahitimu wakiingia ukumbini
Mkuu wa shule ya sekondari Kom,Mwita Waryoba akielezea historia ya shule hiyo
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi akizungumza wakati wa mahafali ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kom
Wahitimu wa kidato cha nne wakipunga mkono
Wahitimu wa kidato cha nne,Scholastica Simon na Dickson Nyansika wakikata keki wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwaka 2017
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimlisha keki mhitimu wa kidato cha nne Dickson Nyansika
Mahafali yanaendelea
Wanafunzi wakiwa wamevaa mavazi mbalimbali ya ubunifu
Wanafunzi wakiimba shairi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ANGALIA PICHA NYINGI ZAIDI ZA MAHAFALI <>
No comments:
Post a Comment