Thursday, November 30, 2017

MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS Nchini akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili kulia) alipowasili kwenye katika Ukumbi wa  Chuo cha Mipango Dodoma tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Mkutano huo unafanyika kwa siku moja leo 30 Novemba, 2017 hapa mjini Dodoma. 

Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS) kimefanya Mkutano wake Mkuu wa Tano wa Mwaka 2017 kwa ufanisi Mkoani Dodoma.
Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini,  Miyuji Dodoma leo Novemba 30,  2017.

Akiongea katika Mkutano huo Kaimu Naibu  Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw.  Charles Malunde kwa niaba ya Naibu Mrajisi ametoa angalizo kwa Vyama vya ushirika nchini kutokufanya biashara za Kibenki nje ya lengo la kuanzishwa kwa SACCOS.

Amesema kuwa katika  vyama vingi vya ushirika uzoefu umeonesha kuwa wakishakuwa na mtaji mkubwa huwa na wazo la kuanzisha Benki, ametoa angalizo kuwa masharti ya uendeshaji wa Benki ni tofauti kabisa na masharti ya uendeshaji wa vyama vya ushirika hivyo ameziasa Saccos zote nchini kutafakari vyema kabla ya kubadili vyama hivyo na kuwa Benki.
“ Ukianzisha Benki huduma za Saccos zitafifia, kumbukeni wateja wa Saccos ni pamoja na wale wa hali ya chini kabisa ikiwa benki hawa huenda mkawaacha” alisisitiza  Kaimu Mrajis Malunde.

Aidha,  amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli zake kwa kufuata sheria  lakini pia kuheshimu na kusikiliza sana wenye mali ambao ni wanachama wa vyama hivyo vya ushirika.
Aliongeza kuwa kwakuwa Mkutano huu utahusisha uchaguzi wa wajumbe wa Bodi Bw. Charles Malunde pia amewaasa Wajumbe wa Mkutano Mkuu kuwa makini katika uchaguzi huo kwa kuchagua watu wenye weledi na wenye mapenzi ya dhati na ushiriki wao ili waweze kutimiza majukumu yanayokusudiwa.

Pia amewataka wagombea wote wanaowania nafasi mbalimbali za chama hicho kujiuliza mambo manne kama ifuatavyo;- Je, watumishi wa Jeshi la Magereza wote ni wanachama? na mnaweka Mkakati gani?, Je wanachama wanaweka akiba za kila mwezi?, Mnajiendesha kisayansi? Mtu akitaka mkopo anapata baada ya muda gani? na swali la mwisho uhusiano na vyama vingine vya ushiriki, SCULT, nje ya nchi ukoje?.

Awali akitoa taarifa ya Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS), Mwenyeki wa Bodi ya Magereza Saccos, DCP. Gideon Nkana amesema kuwa Idadi ya wanachama imeongezeka hadi kufikia wanachama zaidi ya 13,000 ikiwa na mtaji wa zaidi ya bilioni 18.
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(katikati) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS kuingia Ukumbini tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma..
Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha. 
Mjumbe wa Mkutano huo ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera, Naibu Kamishna wa Magereza, Jeremiah Nkondo akichangia mada katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara . 
Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga akitoa neno la shukrani mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo. 
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiteta jambo na Mgeni rasmi Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde kama inavyoonekana katika picha.
Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(waliosimama). Walioketi(wa tatu toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza Saccos anayemaliza muda wake, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili toka kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tano unaofanyika kwa siku moja Mkoani Dodoma(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza).

No comments: