Baadhi ya vikundi vya wajasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe wakati wa sherehe za kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya mikopo ambayo iatawasaidia katika kuendeshea shughuli zao za biashara pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo.
Mkuu wa Wilaya Kisarawe Happiness Seneda aliyesimama akizungumza na vikundi vya wajasiriamali kutoka kata mbali mbali katika halfa fupi ya kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili mkopo wa kuwawezesha kiuchimi.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda akizungumza jambo katika halfa fupi ya vikundi vya wajasiriamali.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashari ya Kisarawe Mussa Gama akizungumza na vikundi vya wajasiriamari hao hawapo pichani kabla ya kukabidhiwa hundi hiyo ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya kuwawezesha mikopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU
……………..
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
HALMASHAURI YA wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoani Pwani katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kuwa na uchumi wa viwanda imetoa kiasi cha shilingi milioni 102 kwa vikundi vya wajasiriamali vipatavyo 49 vya wakinamama,vijana pamoja na walemavu kwa lengo la kuweza kuwasaidia kuendesha shughuli zao mbali mbali za biashara mbali mbali ikiwemo na kuwawezeha ili waweze kujikita zaidi katika kujenga viwanda vidogo vidogo.
Akizungumza katika halfa fupi ya kukabidhi hundi ya fedha hizo iliyohuduriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na viongozi wa vikundi hivyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama alisema kwamba fedha hizo za mikopo zimetolewa kwa vikundi hivyo kutokea kata zote 17 ambapo zimetokana na makusanyo ya mapato ya ndani.
Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kuweza kukuza uchumi wa nchi kutokana na kuweza kuwapa fursa wajarisiamali hao kupania wigo wa kibiashara pamoja na kuanzissha viwanda vingine vidogo vidogo ambayo vitaweza kuongeza upatikanaji wa ajira mpya na kupunguza wimbi la umasikini.
“Kwa kweli sisi kama halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe tumejipanga kuweka mipango madhubuti katika kuviwezesha vikundi vyetu vya ujasiriamali kwa kutumia fedha zetu ambazo zinatokana na makusanyo ya mapato ya nadani, hivyo vikundi hiivi ni moja ya mipango yetu katika kuhakikisha ile asilimia 10 iliyotengwa inawafikia walengwa na kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo,”alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda ameviasa vikundi vyote vilivyopata mkopo huo hususan kwa wakinamama kuachana kabisa na vitendo vya kutumia fedha hizo vibaya kwa shughuli ambazo hazina manufaa yoyote kwa jamii, kama vile kuwachezesha watoto wao ngoma wakati wa kufunga shule pamoja na kununulia madela kitu ambacho amekilaani vikali.
Aidha Seneda alisema kuwa malengo ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha wananchi wake wanawezeshwa kwa namna mbali mbali ikiwemo kuwapatia mikopo ambayo itaweza kuwapa fursa ya kukuza biashara zao pamoja na wengine kufanya biashara zao ndondogo amabzo zitaweza kuwapatia kipato na kujikwamua kiuchumi.
“Jamani mimi kama kiongozi wenu napenda kuwaasa wale wote mlionufaika na mkopo huu, kuhakikisha mnazitumia vizuri fedha hizi hasa kwa upande wa wakinamama ambao wamekuwa na tabia pindi wanapotata pesa wanazitumia katika matumizi mengine ya kununulia madela kwa ajili ya sare pamoja shughuli nyingine kama vile kuwacheza ngoma watoto wao hii tabia kwa kweli sipendi kuiona katika Wilaya yangu,”alisema Seneda.
Nao baadhi ya wajasiriamali ambao wamenufaika na mkopo wa fedha hizo akiwemo Monica Muhoza ambaye ni mlemavu wa miguu, Faudhia Kasikasi, pamoja na Gudluck Akyoo wameshukuru uongozi mzima wa halmashauri ya Kisarawe na kusema kuwa fedha hizo walizopatiwa ni mkombozi mkubwa kwa upande wao kwani zitaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi pamoja na kujikimu kimaisha na kuendesha familia zao.
VIKUNDI hivyo vya wajasiriamali 49 kutoka kata 17 za Wilayani Kisarawe zimewahusiha wakinamama, vijana, pamoja na makundi vya walemavu ambapo vimepata mkopo wa fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 102 ikiwa ni makusanyo ya mapato ya fedha za ndani.
No comments:
Post a Comment