Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akizungumza na wananchi wa Tarime mkoani Mara na kutoa miezi
sita kwa wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kuanzisha madawati ya
ulinzi na usalama kwa mtoto kike katika Shule zao.
Mkuu
Wa mkoa wa Mara Mhe. Charles Mlingwa akihamasisha wananchi wa mkoa wa
Mara kuzingatia na kulinda haki za Mtoto katika Maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Mtoto wa Kike iliyofikia kilele chake 11/10/2017.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akizindua kampeni ya kitaifa ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli
mbiu isemayo:” "Najitambua Elimu ndio Mpango mzima".
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akibonyeza kitufe kuzindua ujumbe wa radio wa kampeni ya kutokomeza
mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” Najitambua Elimu ndio Mpango
Mzima”
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto, wadau na madereva
bodaboda wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara muda mfupi baada ya Maadhimisho
ya Siku ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika kitaifa wilayani Tarime mkoani
Mara. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
Na Mwandishi Wetu Tarime- Mara.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
ametoa miezi sita kwa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini
kuanzisha Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto kwa ajili ya
kusikilizamatatizo ya wanafunzi hasa wanafunzi wa kike.
Akizungumza
wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa KikeKitaifa
iliyofanyika katika wilaya ya Tarime mkoani Maraamewasisitiza wakuu wa
shule za Msingi na Sekondari kuzingatia uwepo wa dawati la ulinzi na
usalama wa mtoto kike katika shule zao ili kuwa salama na kuwa na
mahali pa keleza matatizo yao.
Mhe.
Ummy ameongeza kuwa suala la kumlinda mtoto wa kike ni jukumu la kila
moja katika jamii na kuwapongeza wadau wa maendeleo ya watoto kwa
jitihada zao na kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa wanajamii
kuhusu madhara ya mimba za utotoni, ukeketaji na ukatili dhidi ya
wanawake na watoto.
“
Niwatake wakuuwashule za msingi na Sekondari kuanzisha madawati kwa
ajili ya ulinzi na usalama wa watoto wa kike kwa ajili ya kusikiliza
shida za wanafunzi wa kike na kuwasaidia kutatua shida zao katika ngazi
ya shule”.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Shirika la kutokomeza ukeketaji Tarime Stela
Mgaya amesema kuwa wamefanikisha kuwaondoa mangariba 63 kutokakatika
kazi ya ungariba na kuwatafutia kazi zingine za kujipatia kipato.
Naye
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Watoto Duniani UNICEF Bi. Maniza Zaman
amewasihi viongozi wa dini na wale wa Kimila ambao wana ushawishi
mkubwa kuziongoza jamii zetu kuwaangalia na kuwasaidia watoto wa Kike.
Mwakilishi
Shirika la Plan Tanzania Bi. Martha Lazaro ameishukuru Serikali na
kuahidi kuendelea kutoa ushirikiao katika kutekeleza mipango mbalimbali
ya mtoto hasa wa kike na vihatarishi vinavyopelekea kuharibu maisha yao.
Katika
Maadhimisho ya mwaka huu Serikali imezindua Kampeni ya Kitaifa ya
utokomezaMimba za Utotoni yenye kauli mbiu isemayo:“ Tutokomeze Mimba za
Utotoni; Tufikie Uchumi wa Viwanda". Maadhimidho hayo, Waziri Ummy
ameteua wimbo wa Shule ya Sekondari ya Welwel na Karatu zote za wilayani
Karatu, Arusha kuwa wimbo mahususiutakaotumika kuhamasisha na
kuelimisha jamii kutokomeza mimba za utotini.
No comments:
Post a Comment