Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiwa na Naibu Mawaziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kakunda (kulia) pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za OR TAMISEMI mjini Dodoma na kufanya kikao na Watumishi.Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Joseph kakunda (kushoto) akisaini kitabu mara baada ya kufika Ofisini ‘OfisiyaRais –TAMISEMI’mjini Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Josephat Sinkamba Kandege akisaini kitabu mara baada ya kufika Ofisini, ‘Ofisi ya Rais –TAMISEMI, mjini Dodoma.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma (hawapopichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo, kulia ni Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda
Watumishi wa OR-TAMISEMI wakifuatilia kikao na Waziri pamoja na Naibu Mawaziri (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za TAMISEMI –mjini Dodoma.
Katika picha ya pamoja ni viongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI (katikati) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Selemani Jafo kushoto akifuatiwa na Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege (Afya,Miundombinu,ViwandanaUwekezaji, naSerikalizaMitaa),KatibuMkuu OR-TAMISEMIMhandisiMusa Iyombe, Naibu Katibu Mkuu (Afya) Zainab Chaula na kulia n iNaibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda (Elimu, Maji, Kilimo, MifugonaMaliasili), NaibuKatibuMkuu –ElimuTixonNzunda(Elimu) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu Tanzania (TSC) Winfrida G.Rutaindurwa.
NTEGHENJWA HOSSEAH – TAMISEMI, DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Said Jaffo amesema hatahamisha Mkuu wa Idara wala Kitengo katika Wizara hii lakini atamtengeneza awe kama anavyotaka ili aweze kuendana na kasi ya utendakaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa kikao chake na Watumishi wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara hii ambapo aliambatana na Manaibu Waziri wa OR-TAMISEMI .
Waziri Jaffo alisema kuwa “Siwezi kuhamisha matatizo kutoka eneo kwenda lingine cha msingi ni kuhakikisha tunamtengeneza hapa hapa awe kama tunavyotaka kulingana na mahitaji yetu na aweze kuendana na kasi ya Serikali hii sasa hivi kasi yetu sio ya kutembea bali ni kukimbia na lazima wote twenda pamoja”.
Aliongeza kuwa nahitaji “Consistency of information” kutoka kwa watalaam wanaofahamu vizuri maeneo yao ya kazi sio kila siku unahamisha unaanza na mtu mpya naye anakuwa hana taarifa za kutosha kuhusu kazi za awali hivyo inachukua muda kuanza kwenda sawa kwangu mimi nasema ntamnyoosha yeyote ambaye haendani na viwango vyangu akiwa hapa hapa na si kwingineko”.
Aidha Waziri Jaffo aliwata Watumishi wote kuacha kufanya kazi kwa ulegevu na kuwa makini wakati wote wa kazi kwani ndio inayopeleka kupata ujira wako, kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kutoa huduma bora kwa wananchi, kutokujali muda hivyo kutumia muda mrefu kukamilisha jukumu ulilopewa ama kutorudisha mrejesho wa kazi na kutojali utu wa watu wengine.
“Nataka nione kila mtumishi yuko “busy for something” ili tuweze kuwasaidia Wananchi wetu, na katika hili tutapimana mmoja mmoja katika eneo lake amefanya nini kwa siku, wiki, mwezi mpaka mwaka na yeye mwenyewe atusaidie kujitathmini kuona kama ana umuhimu wowote katika eneo lak ama Lah”
Wizara hii ni Injini ya mabadiliko katika Nchi yetu hivyo sisi lazima tuwe Wizara bora inayofanya kazi zitakazoleta chachu ya Maendeleo kwa mwanancHi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, hivyo nitasughulika na watumishi wote mpaka nione mnaendenda kadiri ya kasi ninayoitaka ili mabadiliko chanya yaweze kutokea alisema waziri Jafo.
“Sitaki kuona mtu anashinda Ofisini Wizara hii ni watekelezaji wa Sera mbalimbali na Sera hizo zinatekelezwa kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa nataka niwaone mkienda kufuatilia utekelezaji na kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa viwango na wananchi wanapata stahiki yao ya huduma bora toka kwenye mamlaka za serikali za mitaa zilizoko kwenye maeneo hayo na sio kushinda Ofisini” Aliongeza Mhe. Jafo.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda amesema ninachohitaji toka kwa watumishi wa OR-TAMISEMI tufanye kazi na tuipende Kazi na kwa pamoja tuweze kuisimamia bajeti ya Serikali ambapo Wizara hii tunapata asilimia 20.7 ya bajeti nzima ya Taifa letu ni lazima tuitendee haki kwa sababu Fedha zinakuja kwetu ni nyingi hii inaonyesha umuhimu wa Wizara hii kwa maendeleo ya taifa.
Amesisitiza mambo matatu anayoyahitaji toka kwa watumishi kuwa ni “clarity” kuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa Majukumu, Sera, Sheria, Program, Miongozo na kanuni mbalimbali sambamba na mazingira wezeshi yatakayomuweza mtumishi kufanya kazi ambayo haya yatatengenezwa na mwajiri pamoja kuwa uwezo wa kufanya kazi ulizopangiwa bila kusimamiwa “competency”.
Naye naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Joseph Sinkamba kandege ninachohitaji zaidi toka kwenu ni ushirikiano kwa sababu hata kama mtu anaweza kiasi gani lazima anahitaji msaada wa mwingine ili aweze kukamilisha kazi yake vizuri hakuna nayeweza peke yake hizi kazi tunategemeana na zaidi ya hapo nahitaji watu wakweli na waaminifu ili tuweze kufikia malengo ya pamoja.
Kikao hiki na watumishi wa TAMISEMI ni cha pili tangu kuapishwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo pamoja na Manaibu Waziri wake Mhe. Mhe. Joseph Sinkamba kandege pamoja na Mhe. George Joseph Kakunda.
TAMISEMI YA WANANCHI

No comments:
Post a Comment