Tuesday, October 24, 2017

VITAMBULISHO VYA TAIFA LULU KWA WANANCHI WA KWIMBA

Wananchi wa Wilayani ya Kwimba wamejitokeza kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi hilo likiendelea. Mpaka sasa idadi kubwa ya wananchi wa Kwimba wameshasajiliwa huku mwitikio wa wananchi ukiongezeka na kuonyesha ni kiu ya wananchi katika kupata Vitambulisho cha Taifa.

Afisa Usajili Wilaya ya Kwimba Ndg Nelson Liyenge amewakumbusha wananchi kujitokeza kwa wingi ili wasajiliwe kwa wakati na kuwawezesha kupata  Vitambulisho vya Taifa. 

 Umati mkubwa wa Wananchi wa wilaya ya Kwimba wakisubiri kuingia kwenye chumba ambacho Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unafanyika. 
 Wananchi wa Wilaya ya Kwimba wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Msimamizi wa Kituo cha Usajili juu ya mambo msingi wanayotakiwa kuzingatia pindi watakapoingia kwenye chumba cha Usajili wakati wa kuchukiliwa alama za kibaiolojia, picha na saini ya kielektroniki. 

Wananchi mbalimbali Wilaya ya Kwimba wakiwa kwenye harakati za Usajili.

Mmoja wa wananchi wa Kwimba akiwa tayari kupigwa picha ikiwa ni sehemu ya hatua za usajili Vitambulisho vya Taifa. 

No comments: