JUMUIYA ya raia wa Comoro waishio Tanzania wameiomba Serikali kupitia Jeshi la Polisi nchini kusaidia kupatikana kwa ndugu yao Ammar Abdousoi Madou (26) aliyepotea na kutoweka kusikojulikana tangu tarehe 29 Juni mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo (jana) Jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Jumuiya hiyo, Larifou Said alisema taarifa za kupotea kwa Madou ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala nchini Uganda ziliifikia familia yake tarehe 29 Juni, mwaka huu.
Said anasema familia ya Madou ilipokea taarifa za kushikiliwa kwa Madou na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha tarehe 27 Juni, mwaka huu kutoka kwa rafiki wa karibu wa Madou anaeishi Mkoani Arusha na baadae kuelezwa kuwa aliachiwa huru tarehe 29 Juni mwaka huu, ingawa tangu kipindi hawajaweza kuonana nae hadi sasa.
Anasema pamoja na familia hiyo kufanya jitihada mbalimbali za kufanikisha upatikanaji wa ndugu yao ikiwemo kufanya Mawasiliano ya mara kwa mara na vyombo vya usalama ikiwemo kuwasiliana na Idara ya upelelezi ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufahamu undani na sababu ya kukamatwa kwa Madou.
Akifafanua zaidi Said anasema Jumuiya hiyo tayari imefanya mawasiliano na Ubalozi wa Komoro nchini, ambao nao uliandika barua katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuelezea malalamiko yao ya kupotea kwa ndugu yao ambapo pamoja na kuomba uchunguzi wa kina uendelee kufanywa na vyombo vya dola vya Tanzania.
“Wiki iliyopita tulielezwa na Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kuwa Madou aliachiwa huru, lakini tulipofunga safari kuelekea Arusha hatukumkuta bado tunaendelea kujenga imani na vyombo vya dola vya Tanzania lakini tunaomba jitihada ziendelee kuongezwa ili Madou aweze kupatikana” alisema Madou.
Akielezea tukio la kukamatwa kwa Madou alisema, ndugu yao alirudi Tanzania mwezi juni mwaka huu kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Idd el fitri ambapo tarehe 27 juni mwaka akiwa njiani kurudi Uganda alikamatwa Moshi Mkoani Kilimanjaro akiwa katika basi yenye namba za Usajili T 502 DHF na baadae kuhamishiwa katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Arusha.
Said anasema pamoja sheria kulitaka Jeshi hilo kumfikisha mtuhuhiwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili, Ofisi ya Polisi ilishindwa kumfikisha mtuhumiwa huyo katika mhimili wa dola na baadae kudai kuwa lilimwachia huru pasipo na kupatikana kwa vielelezo vinavyoonyeshwa kuachiwa kwake.
Mwanasheria wa Jumuiya ya Raia wa Comoro waishio Tanzania, Larifou Said akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu tukio la kupotea kwa Mwanafunzi Raia wa nchi hiyo Ammar Abdousoi Madou (pichani) ambapo waliliomba Jeshi la Polisi kusaidia upatikanaji wa ndugu yao huyo.
Mwanasheria wa Jumuiya ya Raia wa Comoro waishio Tanzania, Larifou Said akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu tukio la kupotea kwa Mwanafunzi Raia wa nchi hiyo Ammar Abdousoi Madou (pichani) ambapo waliliomba Jeshi la Polisi kusaidia upatikanaji wa ndugu yao huyo.
No comments:
Post a Comment