Saturday, October 7, 2017

BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI TANESCO LAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI

BARAZA kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limeazimia kuunga mkono jitihada za Rais Dkt John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya watu wenye kipato cha kati kwa kufanya kazi kwa umahiri,uzalendo na ufanisi.

Akizungumza katika ufungaji wa baraza hilo mwishoni mwa wiki mjini Tanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi alisema bodi hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano katika kuhakikisha shirika linafikia malengo yake muhimu.

Alisema malengo hayo ambayo yanahitajika katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unafikiwa kwa kasi kubwa kutakapotokana na kuwa na umeme wa uhakika ambao unaweza kusukuma gurudumu la maendeleo.Aidha alisisitiza juu ya umuhimu wa utunzaji wa miundombinu ya shirika hilo ili iweze kusaidia kutoa huduma zake wakati wote bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ile.

Hata hivyo aliwaasa wafanyakazi wa shirika hilo kuhakikisha wanakuwa walinzi wa miundombinu hiyo ili isiweze kuibiwa ikiwemo kuhakikisha haihujumiwi na watu wanaoweza kufanya hivyo.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga 
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga 
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt.Tito E. Mwinuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo kulia akiwa na Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale wakisikiliza kwa umakini hoja za wafanyakazi 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi akizungumza katika mkutano huo 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi kushoto akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka wakati wa kikao hicho 
Mwenyekiti wa Tuico Tanzania,Paul Sangeze akizungumza katika mkutano huo 
Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya Afya kwa wajumbe wa baraza hilo 
Mmmoja wa wafanyakazi na mjumbe wa baraza hilo akichangia kwenye mkutano huo 
mmoja wa wajumbe wa baraza hilo Janet Vesso akichangia mada 
Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi wa pili kutoka kushoto,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka kulia na Mwenyekiti wa TUICO Taifa Paul Sangeze wa kwanza kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale

No comments: