Waziri
wa kazi, ajira, sera, bunge, vijana na wenye ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama amelipongeza Shirika la NSSF kwa kuwa mfano wa kuigwa katika
nyanja za kiuchumi na kijamii. Waziri mkuu aliyasema hayo katika mkutano
wa wadau wa NSSF unaoendelea katika Kituo cha kimataifa cha mikutano
AICC, Arusha
Waziri
wa kazi pia alipongeza NSSF kwa kuandaa mkutano wa wadau unaofanyika
hapa jijini Arusha, alisema mkutano huo siyo muhimu kwa NSSF na wadau tu
bali pia kwa maendeleo na ustawi wa Taifa letu. Pia alifurahi kupata
nafasi ya kufuatilia utendaji wa NSSF pamoja na kuona moja kwa moja
kutoka kwa wadau wa NSSF.
Pia
aliwapongeza wadau wa NSSF kwa kuitikia wito wake wa kuja kushiriki
ili kupata taarifa za utekelezaji wa maazimio waliyokubaliana mwaka
jana, taarifa za utendaji na kuchangia mawazo yatakayoleta tija ya
kulijenga Shirika. Aidha, aliwapongeza Wageni mbalimbali katika mkutano
huo ambao ni pamoja na Mhe. Anthony Mavunde, Katibu Mkuu Ndg. Eric
Shitindi, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA na Wakurugenzi wa Mifuko mingine ya
Pensheni.
Vile
vile Waziri wa kazi alitoa pongezi kubwa kwa namna ambavyo NSSF
ilivyojitolea katika kutekeleza jukumu la kukuza Uchumi wa Viwanda
kwani alisema Ujenzi wa Taifa si jukumu la Serikali Kuu peke yake bali
ni la kila Mtanzania mmoja mmoja, taasisi na makampuni, na ndio maana
NSSF pamoja na kuwa na jukumu la hifadhi ya jamii kwa mujibu ya sheria
yake husika, imeona haja ya kupanua wigo wa uwekezaji wake na kuelekea
katika viwanda jambo ambalo litaongeza ajira, kuongeza uzalishaji, na
kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Waziri
Mhagama alitoa mfano katika uwekezaji wa NSSF katika kukuza viwanda
tumeshuhudia uwezekano wa kuzalisha ajira za moja kwa moja kwa
Watanzania kutoka na uwekezaji ilioufanya katika viwanda mbali mbali.
Nichukue fursa hii kuipongeza NSSF kwa kutoa mkopo wa shilingi bilioni
3.1 kwa lengo la kuongeza uzalishaji katika kiwanda cha madawa kilichopo
Kibaha chini ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Katika kiwanda
hiki ambapo ajira 100 zimezalishwa. Uzalishaji wa viuadudu ulianza Mwezi
Desemba 2016 na mpaka sasa kiwanda kimezalisha jumla ya lita 327,400
ambazo ziliuzwa katika masoko ya ndani na nje.
Shirika
lilitoa Mkopo kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanda cha Chaki kilicho chini
ya Usimamizi wa Halmashauri ya Maswa, Mkoani Simiyu mnamo mwezi June,
2017. Mkopo huu kwa ujumla utaongeza uzalishaji wa chaki kutokea vipande
432,000 vya chaki nyeupe (sawa na Katoni 180) kwa siku hadi vipande
milioni 4.8 vya chaki nyeupe na za rangi (sawa na Katoni 2,000) kwa
siku. Ongezeko la uzalishaji huu wa chaki utasaidia kuendeleza Sera ya
Serikali ya “Elimu Bila Malipo” kwani itasaidia kupunguza mahitaji
makubwa ya chaki katika shule za awali na msingi. Jumla ya Ajira 100 za
moja kwa moja zinatarajiwa kutokana na uwekezaji huu.
Pia
aliwapongeza NSSF kwa kushirikiana na PPF, na Jeshi la Magereza kupitia
Kampuni ya Mkulazi, wamewekeza katika Mradi mkubwa wa shamba la miwa na
Kiwanda cha Sukari kilichopo Mbigiri ambapo tayari hatua za upandaji
miwa zimeanza nami nikiwa miongoni mwa watu waliopata fursa ya kupanda
miwa ya
mwanzo
kabisa. Kiwanda hiki Cha Mbigiri kitakapokamilika kinatarajiwa
kuzalisha tani 50,000 za sukari kwa mwaka. Mpaka sasa mradi huu
umezalisha ajira 300 za moja kwa moja na pia kupitia mpango wake wa
wakulima wa nje katika eneo la Dakawa, imeweza kuandikisha jumla ya
wakulima 1,500 wanaotegemewa kuanza kilimo cha miwa kuanzia mwezi
Novemba, 2017 ambao watalima heka 15,297.
No comments:
Post a Comment