Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akikagua ofisi za Idara ya uhariri na uchapishaji alipotembelea ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kukagua na kuona shughuli zinazofanywa na Baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji BAKITA Dkt. Suleman Sewangi
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akikagua jengo lililokua likitumiwa na waliokua watumishi wa Bima baada ya watu hao kuondolewa katika majengo hayo kupisha ofisi za BAKITA leo wakati wa ziara yake BAKITA Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji BAKITA Dkt. Suleman Sewangi
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akikagua vifaa vinavyotumika kuhariri taarifa mbalimbali zinazowashilishwa BAKITA wakati wa ziara yake katika ofisi za BAKITA kuona namna ofisi hiyo inavyofanya kazi. Mwenye miwani ni Katibu Mtendaji BAKITA Dkt. Suleman Sewangi
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akipokea kamusi kutika kwa mtumishi wa BAKITA Bibi. Wema Msigwa alipofanya ziara katika ofisi za BAKITA leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji BAKITA Dkt. Suleman Sewangi
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba (kulia) alipofanya ziara TCRA kuangalia namna taasisi hiyo inavyosimamia maudhui ya vyombo vya habari nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba (katikati) akizungumza alipomtembeza Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza kuangalia gari lililofungwa mtambo wa kusimamia masafa ya redio nchini wakati wa ziara yake TCRA leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Posta TCRA Bibi. Cecilia Mkoba (kulia) akimuelezea Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) namna mawasiliano zamani yalivyokuwa yakifikishwa kutoka eneo moja kwenda eneo lingine alipotembelea makumbusho ya mawasiliano leo wakati wa ziara yake TCRA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba (kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) alipotembelea Idara inayosimamia maudhui ya televisheni zote nchini wakati wa ziara yake TCRA leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akizungumza na menejimenti ya TCRA alipofanya ziara katika Taasisi hiyo kuangalia namna inavyosimamia maudhui ya vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba.
Picha zote na Genofeva Matemu -WHUSM
No comments:
Post a Comment