Na Veronica Simba - Dodoma
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amefanya ziara katika Kituo cha
kupoza na kusambaza umeme kilichopo eneo la Zuzu mjini Dodoma, leo
Oktoba 28, 2017.
Akiwa amefuatana na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu, Naibu Waziri Mgalu, ametembelea Kituo
hicho ili kujionea utendaji kazi wake.
Akitoa malelezo kwa Naibu Waziri, Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Bosco
Mgina amesema kuwa, Kituo hupokea msongo wa umeme wa kilivolti 220
katika njia tatu ambazo ni Mtera, Iringa One na Iringa Two.
Aidha, ameongeza kuwa, Kituo kina transfoma mbili za kupoza umeme
ambapo kila moja ina uwezo wa kutoa megawati 24 za umeme hivyo
kufanya jumla yake kuwa megawati 48.
Akizungumzia hali ya upatikanaji wa umeme kwa Mkoa wa Dodoma,
Meneja Temu ameeleza kuwa kwa sasa huduma ya nishati hiyo muhimu
imerejea katika maeneo yote baada ya jitihada za Shirika hilo katika
kutatua matatizo yaliyojitokeza hivi karibuni.
Akihitimisha ziara yake katika Kituo hicho, Naibu Waziri Mgalu
amewasisitiza viongozi wa TANESCO kuhakikisha huduma ya umeme wa
uhakika inaendelea kutolewa kwa wateja katika maeneo yote.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kushoto), akisikiliza
maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza
umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kulia) kuhusu utendaji
kazi wa Kituo hicho. Wengine pichani (kutoka kushoto) ni Msaidizi wa
Naibu Waziri, Ngereja Mgejwa, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma,
Zakayo Temu na Mwendeshaji wa Mitambo katika Kituo hicho, Benedict
Stephano.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), akiangalia kwa makini,
kupitia Kompyuta, namna umeme unavyopokelewa katika Kituo cha
kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu, Dodoma na kusambazwa kwa
wateja. Anayetoa maelezo (kulia) ni Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Bosco
Mgina. Katikati ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu
mjini Dodoma, Bosco Mgina (kushoto), akimwonesha Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu (kulia), namna umeme unavyopokelewa kituoni hapo
na kusambazwa kwa wateja.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kushoto), akisisitiza
jambo kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme
kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kulia). Wengine pichani ni
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu (wa pili kutoka
kulia), Msaidizi wa Naibu Waziri, Ngereja Mgejwa (wa pili kutoka kushoto)
na Mwendeshaji wa Mitambo katika Kituo hicho, Benedict Stephano.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu (wa pili kutoka
kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili
kutoka kushoto), wakati Naibu Waziri alipotembelea Kituo hicho kujionea
utendaji kazi wake. Wengine pichani ni Kaimu Mkuu wa Kituo hicho Bosco
Mgina (kulia) na Mwendeshaji wa Mitambo katika Kituo hicho, Benedict
Stephano.
Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu
mjini Dodoma, Bosco Mgina (kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri
wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), wakati Naibu Waziri alipotembelea
Kituo hicho kujionea utendaji kazi wake. Kulia ni Meneja wa TANESCO
Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), akiwa katika ziara ya
kukagua Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini
Dodoma. Kulia ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), akitoa maelekezo kwa
Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu
mjini Dodoma, Bosco Mgina (kulia), alipotembelea Kituo hicho kujionea
utendaji kazi wake. Kushoto ni Meneja wa TANESCO wa Mkoa wa
Dodoma, Zakayo Temu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), akikagua Kituo cha
kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma. Kushoto ni
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu na kulia ni Kaimu
Mkuu wa Kituo hicho, Bosco Mgina.
No comments:
Post a Comment