Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha wakimsikiliza Mkuu wa idara ya Kilimo ya halmashauri ya Meru,Grace Solomon kwenye kilele cha siku tatu za maonesho ya Jukwaa la Wakulima Meru(Juwame) eneo la Leganga.
Meneja kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kushoto) na Mkuu Idara ya Kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Grace Solomon(katikati) wakimkabidhi zawadi ya baiskeli yenye boksi maalumu la kubebea pembejeo mkulima bora kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji ya Nanenane mwaka huu kutoka mkoa wa Kilimanjaro,Ebenezer Shao .
Mkulima ambaye ameandaa mashamba darasa mengi kwaajili ya kutoa elimu kwa wakulima wilayani Arumeru,Letayo Nnko akiwa na baskeli aliyokabidhiwa.
Meneja kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kushoto) na Mkuu Idara ya Kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Grace Solomon(katikati) wakimkabidhi zawadi ya baiskeli yenye boksi maalumu la kubebea pembejeo mkulima bora kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji ya Nanenane mwaka huu kutoka mkoa wa Arusha,Kaanael Kitomary .
Wananchi wakijifunza mbinu bora za kilimo kutoka kwenye mabanda yaliyoandaliwakuwahudumia wakulima.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
Arusha.Kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini imewatambua kwa kuwapa zawadi wakulima bora watatu waliotangazwa washindi kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji ya Nanenane kanda ya Kaskazini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Themi jijini hapa mwezi Agosti mwaka huu na mkulima mmoja aliyeongoza kwa kuandaa mashamba darasa.
Meneja Kiongozi wa kampuni hiyo nchini,Frank Wenga alisema wameamua kutoa zawadi za baiskeli zenye boksi maalumu la kubebea pembejeo wakati wa kilele cha Jukwaa la Wakulima Meru (Juwame) baada ya kutambua uwezo wao katika kilimo cha kisasa kinachozingatia kanuni za matumizi ya mbegu bora.
"Kampuni yetu inawapongeza kwa kuonesha mfano wa kuigwa katika mikoa yenu,naamini wakulima wengine wataiga mbinu sahihi za kilimo mnazotumia kufikia malengo hadi kutambuliwa kwenye maonesho ya kanda ya kaskazini kama wakulima bora nasi tukiwa wadau tunawapongeza,"alisema Wenga
Walionufaika na baiskeli hizo zenye thamani ya Sh 1.2 milioni ni mkulima bora kutoka mkoa wa Kilimanjaro ni Ebenezeri Shao,Kaanael Kitomari kutoka mkoa wa Arusha, Boay Tlem mkoa wa Manyara na Letayo Nnko mkulima kutoka halmashauri ya Meru ambaye ameandaa mashamba darasa mengi zaidi kwaajili ya kutoa elimu kwa wakulima wenzake.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa baiskeli hiyo,Nnko alisema itamsaidia katika shughuli za kilimo na kuishukuru kampuni ya Monsanto kwa kutambua juhudi zake za kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa usalama wa chakula.Awali Mkuu wa idara ya kilimo katika halmashauri ya Meru,Grace Solomoni alisema wakulima wamekua wakipata changamoto ya kupata mbegu bora kwa wakati na wakati mwingine wamejikuta wakinunua mbegu bandia na kupata hasara.
Aliwataka wafanyabiashara wa makampuni ya mbegu kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora kwa wakati ili kuwawezesha kuwa na kilimo chenye tija na sio kulima kwa mazoea kwaajili ya kujikimu tu.
No comments:
Post a Comment