Saturday, October 28, 2017

DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA

Na Mathias Canal, Arusha

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) leo Octoba 28, 2017 amekipongeza Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) kwa kuendelea kufungua matawi mengi nchini ya kuuza pembejeo bora za kilimo.
Mhe Mwanjelwa ametoa pongezi hizo wakati akihutubia kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Tanganyika Farmers’ association (TFA) uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha.
Alisema kuwa hiyo ni ishara njema ya kuunga mkono Ilani ya Chama cha Mapinduzi na juhudi za Serikali katika kuendeleza Sekta za kiuchumi ambazo ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Alisema kuwa Kwa wajibu huo, Wizara ya kilimo imeona juhudi kubwa na za makusudi za  Kampuni ya TFA jinsi ilivyojipanga katika kuwahudumia Wananchi na Wakulima nchini.
Kupitia Mkutano huo Aliwaomba Wananchi wote kuendelea kuiunga mkono Kampuni ya TFA ili waweze kupata maendeleo ya haraka kwa kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo ili kuondokana na kilimo cha mazoea na kuingia katika kilimo cha kisasa.
Mheshimiwa Dkt Mwanjelwa alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imetoa msukumo mkubwa katika  kuendeleza Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na hasa kwa kuzingatia kuwa nchi imeaanza safari ya kuelekea kwenye uchumi wa Viwanda ambao unazitegemea Sekta hizo kama chanzo cha malighafi kwa ajili ya kuziongeza thamani bidhaa lakini pia kuzisindika kwa ajili ya biashara katika soko la ndani na nje.
Alitoa Rai kwa Wananchi wote na Wanachama wa TFA kutumia vizuri mtandao wa Mawakala wa TFA, kwani inalenga kumuondolea Mkulima matatizo ya upatikanaji na matumizi ya pembejeo hafifu za kilimo.

Alisema hiyo ndiyo ishara ya kuifanya TFA iweze kuendelea kutoa huduma zake kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.

“Nichukue fursa hii nafasi hii kuwakumbusha wanachama wa TFA na Wananchi kwa ujumla kuwa, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amedhamiria kuendeleza Viwanda vilivyopo hapa nchini, na kuanziasha vipya, nanyi kama Wabia, Wadau wa Wakulima katika kuchangia maendeleo ya viwanda hivyo, natoa rai kwenu kuendelea kukithamini kilimo kwa kuongeza tija na uzalishaji, ili viwanda vilivyopo na vitakavyoanzishwa viweze kupata malighafi na rasilimali zakutosha na hatimaye tufikie kwenye uchumi wa kati” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Mhe Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa alisema kuwa Wizara ya Kilimo imeamua kuweka utaratibu wa kununua mbolea hapa nchini kupitia Mfumo wa Ununuaji wa Pamoja ya “Bulk Procurement System - BPS” na wakati huohuo kuanzisha Mfumo wa Kuuza Mbolea kwa bei Elekezi, ambapo kwa sehemu kubwa ya nchi mbolea imeshuka kwa zaidi ya asilimia 30.
Mfumo huo unalenga kupunguza kero ya upatikanaji na ulanguzi katika bei za mbolea. Kupitia mfumo huo, Serikali inaamini matumizi ya mbolea hapa nchini yataongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita, na kuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya kilimo.
Huduma zinazotolewa na TFA ni kuuza Zana bora za kilimo, Pembejeo za kilimo kama Mbolea, Mbegu bora, Viuwatilifu mbalimbali pamoja na kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa Wakulima, kama juhudi ya kumpunguzia mkulima, mmekuwa mkiagiza baadhi ya pembejeo toka nje ya nchi kwa kuzingatia sheria na taratibu zote.  Nawapongeza kwa jinsi mlivyojipanga vema katika kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Kilimo.
Katika Mkutano huo hoja mbalimbali zimeibuka kutoka kwa wanachama ikiwemo Ongezeko la gharama za mahindi katika Mkoa wa Njombe hoja ambayo Mhe Naibu Waziri ameahidi kuzuru Mkoani Mbeya kufatilia jambo hilo.
Aidha, Baadhi ya wanachama wamempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kufuta 
Jumla ya tozo 80 ambapo kati ya tozo 139 zimefutwa na tozo nne (4) zimepunguzwa viwango. Tozo, kodi na ada zinajumuisha  kufutwa kwa tozo kumi (10) na mbili (2) kupunguza viwango kwenye zao la tumbaku.  Kwenye zao la kahawa zimefutwa tozo 17 na moja (1) kupunguzwa kiwango; sukari zimefutwa 16; pamba tozo zilizofutwa ni mbili (2); kwenye korosho tozo mbili zimefutwa na chai imefutwa tozo moja (1).
Katika kuongeza upatikanaji wa pembejeo tozo tatu (3) zimefutwa na moja (1) imepunguzwa kiwango kwenye mbolea na  tozo saba (7) zilizokuwa kwenye mbegu nazo zimefutwa. Katika Ushirika jumla ya tozo 20 zimefutwa katika ngazi mbalimbali.
 Mgeni Rasmi- Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha. Picha zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akishiriki sala ya kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Wanachama wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) wakifatilia Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha, leo Octoba 28, 2017.
  Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro akitoa salamu za Mkoa muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mkazi wa Moshi Mkoani Kilimanjaro ambaye ni Mwanachama wa TFA Shekh Ally Mwamba akiongoza wanachama wa TFA kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Katibu wa Kampuni ya TFA na Ofisi ya kisheria Bi Pendo Jacob mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), Mwingine ni Bi Cathy Elizabeth S. Long'lway. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo kuhusu Kazi za TFA banda la TFA mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TFA Ndg Peter Ezrah Sirikikwa, na kushoto kwake ni Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.

 Mwanachama wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) Bi Mwanahamisi Salim Bakari akitoa shukrani zake kwa Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha, leo Octoba 28, 2017.


Picha ya pamoja Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb), Mwenyekiti wa TFA Ndg Peter Ezrah Sirikikwa, Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro na viongozi wengine wa TFA mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha, leo Octoba 28, 2017. 

No comments: