Katibu wa sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma Bw. Xavier Daudi akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki jinsi ya ufanyaji kazi wa menejimenti hiyo katika uzinduzi wa Bodi mpya uliofanyika leo katika Maktaba Kuu ya Taifa Jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki na pili kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro akitoa salama na kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi Sekritarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa ofisi hiyo uliofanyika Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kutoa kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki na pili kushoto ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akihutubia katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Sekritarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa ofisi hiyo uliofanyika Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro.
Mwenyekti wa Bodi mpya ya Sekritarieti ya Ajira katika utumishi wa umma Bi.Rose Lugembe katika uzinduzi wa tatu wa bodi pamoja na mkataba wa huduma kwa mteja uliofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kulia ni moja ya wajumbe wa bodi hiyo Bw.Mbaraka Abdul Wakill.Picha na Paschal Dotto-MAELEZO
Na Thobias Robert- MAELEZO
Bodi mpya ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetakiwa kusimamia vyema majukumu yake ya upatikanaji wa rasimali watu wenye weledi, sifa na haiba ambao wataisaidia serikali katika kufikia azma yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025.
Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Angelah Kairuki alipokuwa akizindua bodi hiyo Jijini Dar es Salaam na kuitaka kuendesha kazi zake kwa uwazi na kwa kuzingatia Sheria kanuni na taratibu.
“Mmeteuliwa katika kipindi cha miaka michache kabla ya Taifa letu kufikia mwaka 2025 ambapo tunalenga kuingia kwenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda hivyo mnalo jukumu kubwa la kulipatia taifa rasilimali watu yenye uwezo wa kutuwezesha kutimiza malengo hayo,” alifafanua Waziri Kairuki.
Waziri Kairuki alisema kuwa, katika kutekeleza majukumu yake bodi haina budi kutenda haki ili kuepuka malalamiko ya upendeleo wa aina yoyote, kujuana, ukabila, na ukanda ambavyo vimekuwa vikitolewa dhidi ya bodi ya Sekrtarieti ya Ajira,na kuwataka kuandaa mpango mkakati ambao ukitumika kila mwombaji wa ajira ataridhika.
Aidha, Mh.Kairuki alisema kuwa, bodi inapaswa kusimamia Sheria, taratibu na kanuni za ajira zilizowekwa hapa nchini ili kulisaidia taifa kupata nguvu kazi itakayokidhi mahitaji ya waajiri na ambayo italisaidia taifa kupiga hatua za kimaendeleo.
“Ili kutekeleza kwa vitendo falsafa ya HAPA KAZI TU, Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga utamaduni wa watu kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi kwa bidii, weledi, na kuzingatia maadili. Hivyo ni wajibu wa Wajumbe wa Bodi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha azma hii kwa kuisaidia serikali kupata watumishi waadilifu,” alisisitiza Waziri Kairuki.
Mh. Kairuki amesema kuwa Sekrtarieti hiyo haina budi kutumia njia za kiteknolojia ili kuwafikia waombaji wengi wa nafasi za kazi waliosambaa kote nchini ili kuwapunguzia gharama za kupeleka maombi yao makao makuu pekee yake, na wakati wa kufanya usaili ambapo waombaji wa mikoani wanalazimika kuja Dar es Salaam, hivyo akashauri usaili uwe unafanyika katika ngazi za mikoa.
Awali akisoma taarifa ya utendaji na utekelezaji wa majukumu wa taasisi hiyo Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi alieleza kuwa, tangu kuanzishwa kwake, taasisi imefanikiwa kujenga mifumo ya mbalimbali ya TEHAMA kwa lengo la kurahisisha uapashanaji wa habari na kuboresha mchakato wa ajira na kurahisisha utendaji kazi.
Aidha Sekretarieti hiyo imefungua tovuti ya ajira (www.ajira.go.tz) , pamoja na kurasa katika mitandaio ya kijamii kama vile facebook, twitter na youtube kwa lengo la kuapanua wigo wa mawasiliano kwa waajiri na waombaji wa ajira hapa nchini.
Alieleza kuwa taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kuwasiliana na vyuo vya elimu ya juu na vyuo vingine ili kuwa naidadi ya wanafunzi wanaohitimu vyuoni hivyo kurahisisha usaili paindi ajira zinapotangazwa.
“Kukua kwa teknolojia nchini na duniani kumewafanya baadhi ya wadau kuitumia vibaya mitandao hasa ile ya kijamii hadi kufikia hatua ya baadhi ya watu kwa utashi wao usiojali maslahi ya serikali na wananchi na kuamua kuandaa matangazo ya uongo kwa kujifanya Sekretarieti imetangaza ajira kwa kutumia mitandao ya kijamii jambo ambalo ni upotoshaji,” alieleza Bw. Daudi kama changamoto inayoikumba taasisi hiyo.
Kwa uapnde wake Mwenyekiti mteulie wa bodi hiyo Bi. Rose Lugembe alileza kuwa, watafanya kazi kwa umakini, weledi pamoja na kuzingatia maadili ya kazi ili kurahisisha upatikanaji wa rasilimali watu.
Bodi hii ni yata tu tangu kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira mwaka 2009, sekretarieti hii ilianzishwa kwa lengo la kuendesha mchakato wa ajira katika utumishi wa Umma ili kuziwezesha mamlaka za ajira kupata nafasi ya kutekeleza majukumu yake ya msingi kama yalivyoainishwa katika hati zinazoanzisha taasisi hizo.
No comments:
Post a Comment