BENKI
ya biashara inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania Investment Bank
(TIB) inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kibenki zenye ubunifu wa
hali ya juu ili kufikia dira ya kuwa benki ambayo ni chaguo la wateja.
Hayo
yamesemwa ka Mkurugenzi mtendaji wa benki ya TIB, Frank Nyabundege
wakati akizungumza na wateja wa benki ya TIB waliofika katika tawi la
Samora jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa benki hiyo inatoa huduma
za TIB mobile, Utoaji wa bure wa dhamana za kibenki, sms alert, Premier
banking, uboreshaji wa kazi za ATM, kutua huduma masaa 24 ya katika tawi
la bandari, huduma za malipo ya kodo kirahisi pamoja na JIPANGE Plan.
Amesema
kuwa "Huu ni mwaka ni waka wetu wa pili tangia kupata kibali cha kutoa
huduma za kibenki na kuendelea kujenga uwezo wa kuwapa wateja huduma za
kipekee."
Amesema kuwa hudum nzuri kwa wateja ndio kipaumbele katika maendeleo ya benki hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya TIB, Frank Mwabundege akihudumia wateja ikiwa ni
wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba
duniani kote.
Wafanyakazi
wa benki ya TIB wakiwahudumia wateja wa waliofika katika benki hiyo
jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba duniani kote.
Mteja
wa benki ya TIB, Irene Kiwia akizungumza na Michuzi TV jijini Dar es
Salaam leo wakati alipofika katika benki ya TIB jijini Dar es Salaam
wakati wa kuwashukuru wateja wa benki hiyo.
Mkuu
wa masoko na mahusiano wa Benki ya TIB, Theresia Soka akizungumza na
wateja pamoja na wafanyakazi wa benki ya TIB waliofika katika benki hiyo
jijini Dar es Salaam leo.
Amewashukuru
wateja wa benki hiyo kufka katika taw la Samora kwaajili ya
kusheherekea pamoja wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuwaomba kutoa
maoni yao ili kwenye mapungufu wajirekebisha.
Baadhi
ya wateja na wafanyakazi wa benki ya TIB wakiwa katika hafla fupi ya
kuwashukuru wateja wao katika wiki ya huduma kwa wateja.
Mteja
wa benki ya TIB, Irene Kiwia pamoja na wateja wengine wakishirikiana
kukata keki kwaajili ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo
hufanyika kila mwaka Oktoba.
Mkuu
wa masoko na mahusiano wa Benki ya TIB, Theresia Soka akikatakata keki
kwaajili ya kulishwa wateja wa benki ya TIB jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya TIB, Frank Nyabundege akimlisha keki Mteja wa
benki ya TIB, Irene Kiwia ikiwa ni kuadhmisha wiki ya huduma kwa wateja
ambayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya Oktoba kila mwaka.
Kushoto ni Mfanyakazi mstaafu wa benki ya TIB akilishwa keki jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja.
Kushoto ni Mfanyakazi mstaafu wa benki ya TIB akilishwa keki jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja.
Baadhi
ya wateja wa benki ya TIB wakilishwa keki jijini Dar es Salaam leo
ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila
wiki ya kwanza ya Oktoba kila mwaka.
Mkurugenzi
wa Mikopo wa Benki ya TIB, Adolphina William akimpa zawadi mteja wa
benki ya TIB kutoka jijini Mbeya na mmiliki wa Kampuni ya GDM Ltd,
Grivas Mwangoka.
Mkurugenzi
wa biashara wa benki ya TIB, Mwallu Mwachang'a akizungumza na wateja
pamoja na kuwashukuru kufuka katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar
es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo
hufanyika Kila Oktoba kila mwaka duniani kote.
Meneja
wa tawi la benki ya TIB tawi la Samora, Philipo Pilla akiwashukuru
wateja wa wa benki ya TIB na waendelee kufurahia huduma za benki ya TIB.
No comments:
Post a Comment