Kamishna
wa Polisi Mussa Ali Mussa, akiwa amebeba mfano wa picha ya ndege wa
kuashiria amani, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP),
Simon Sirro ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya
Amani Duniani-Tanzania yaliyofanyika leo Viwanja vya Mwembe Yanga jijini
Dar es Salaam.
Maandamano ya kuadhimisha siku hiyo yakifanyika.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wawakilishi mbalimbali na viongozi wa dini wakiwa wamebeba mfano wa ndege huyo.
Maadhimisho yakiendelea.
Sheikh Hemed Bin Jalala akizungumzia umuhimu wa amani nchini
Afisa Habari Kitengo Cha Habari cha Umoja wa Mataifa-UNIC, Stella Vuzo, akizungumzia ushiriki wa UNIC katika kudumisha amani.
Wanahabari wakiwa kazini katika maadhimisho hayo.
Wananchi wakishuhudia maadhimisho hayo.
Wasanii wakionesha umahiri wa kucheza na nyoka katika maadhimisho hayo.
Kiongozi
wa Chama cha Scout Tanzania, Kamishna Mkuu Msaidizi Kazi Maalum, Mary
Anyitike akiwa na vijana wake kwenye maadhimisho hayo.
Mwakilishi
wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la UN linaloshughulikia
wahamiaji la IOM, Dk. Quasim Sufi, akihutubia. Kutoka kulia ni Kamishna
Mwandamizi wa Polisi, Suzan Kaganda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam SACP, Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke,
Kamishna Msaidizi (ACP), Emanuel Lukuya na Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa.
Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa, akihutubia.
Maadhimisho yakifanyika
Scout wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi mbalimbali.
Na Dotto Mwaibale
VIJANA
wametakiwa wasipishane na fursa kwa kwenda nchi ya nchi kuzitafuta
wakati wenzao wa nchi hizo wakija kunufaika nazo hapa nchini.
Rai
hiyo imetolewa na Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa wakati akihutubia
kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani-Tanzania
yaliyofanyika leo Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
"Vijana
acheni mipango ya kwenda kuzitafuta fursa nje ya nchi kwani wenzenu
kutoka nchi hizo wamekuwa wakija kunufaika nazo hapa nchini" alisema
Mussa.
Alisema
serikali imeweka mazingira mazuri hivyo ni vizuri hali hiyo ikatumika
kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo hasa katika wakati huu nchi
ikiingia katika uchumi wa viwanda.
Aliwataka wazazi na walezi kutoa malezi bora kwa watoto wao ili kuwaepusha kujiingiza katika makundi yasiofaa.
Aliwataka wazazi na walezi kutoa malezi bora kwa watoto wao ili kuwaepusha kujiingiza katika makundi yasiofaa.
Katika
hatua nyingine Kamishna Mussa alisema amani ya nchi itadumishwa na kila
mtu na kuwa watu waondoe dhana ya kuwa amani hiyo italetwa na vyombo
vya dola ikiwemo polisi.
Alisema
suala la amani si la mtu mmoja bali ni la kila mtu jeshi la polisi kazi
yake ni kuilinda na kumkamata mtu yeyote anayeonekana kusababisha
viashiria vya kutoweka kwa amani hiyo.
Mwakilishi
wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la UN linaloshughulikia
wahamiaji la IOM, Dk. Quasim Sufi alisema amani ni jambo la muhimu kwa
nchi na mustakari wa maendeleo.
Alisema
bila ya amani hakuna kitu kitakacho weza kufanyika na ndio maana UN
imekuwa ikisisitiza amani duniani kote.Sheikh Hemed Bin Jalala alisema
amani ndiyo msingi wa dini zote ya kiislam na kikristo na kuwa amani
haipaswi kuchezewa kwani ndio neema tuliyopewa na mwenyezi mungu.
Jalala
alisema amani ni msingi wa dini uliojengwa kiimani na kutakiwa
kuihubiri na kuwa wale wanaohubiri vita na machafuko wanatoka katika
dini ya mashetani.Afisa Habari Kitemgo Cha Habari cha Umoja wa
Mataifa-UNIC, Stella Vuzo aliwataka vijana kuendelea kuidumisha amani
iliyopo nchini kwani wao ndio rahisi kurubuniwa kutokana na kuwa wengi.
"Katika
maadhimisho ya siku ya amani duniani tunapenda kuwashirikisha vijana
kutokana na wingi na umuhimu wao katika kutunza amani" alisema
Vuzo.Alisema vijana watumie fursa ya amani iliyopo nchini katika kufanya
shughuli zao za maendeleo badala ya kukaa bure.
Vuzo alisema Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni " Pamoja Katika Kudumisha Amani: Heshima, Usalama na Utu kwa wote"
Maadhimisho hayo yameandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na taasisi mbalimbali kama Global Peace Tanzania, Global Network of Religions for Children- GNRC, Chama cha Scout Tanzania, Asasi ya Vijana wa Umoja wa mataifa YUNA Tanzania, wanafunzi na wananchi.
No comments:
Post a Comment