Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili
kushoto) akiwasili na kupokelewa na Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye (kulia) wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na
Utamaduni la kimataifa Bagamoyo Jana katika Taasisi hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya
ushauri ya TaSUBa Bw. George Yambesi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili
kulia) akimsikiliza mjasiriamali wa kazi za sanaa kutoka Dar es Salaam Bibi. Magreth Kabonge
(kushoto) alipotembelea banda lake kabla ya kufungua Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni
la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa. Kulia ni Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa
na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia)
akiangalia moja ya kazi za sanaa iliyotengenezwa na mbunifu kutoka Arusha Bi. Joyce Lema
(kushoto) alipotembelea banda lake kabla ya kufungua Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni
la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia)
akionyesha picha yenye mfano wa sura yake iliyochorwa na kalamu ya risasi na mwanafunzi
kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. Baraka Jeje (kushoto)
alipotembelea banda lake kabla ya kufungua Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la
kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
wakiimba wimbo wa taifa wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la
kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi hiyo.
Wanafunzi kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wakicheza ngoma
wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana
katika Taasisi hiyo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa
Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu
kulia) akishirikiana na Mtendaji Mkuu kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Dkt.
Herbert Makoye (wapili kulia), Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Erica Yegelea (watatu
kushoto), Mtendaji Mkuu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (kulia) na
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mhe. Shukuru Kawambwa (wapili kushoto) kukata keki
kuashiria uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana
katika Taasisi ya TaSUBa.
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeagizwa
kukaa na kufanya tathmini ya kina kuandaa mpango mkakati mzuri wa namna ya
kuliendesha tamasha la Sanaa na Utamaduni ili liweze kuwa na tija zaidi kwa wasanii
na Taasisi kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la
kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi hiyo mjini Bagomoyo.
“Tangu kuanzishwa kwa tamasha hili mwaka 1982, Tamasha limeendelea kuwa kivutio
kikubwa kwa wasanii na wadau wa sanaa ndani na nje ya nchi na wananchi kwa
ujumla hivyo ni vyema Bodi ya ushauri ya TaSUBa ikapanga mikakati yenye tija zaidi
kwa maslahi ya wasanii wetu na Taasisi yetu” amesema Mhe. Mwakyembe.
Aidha Mhe. Mwakyembe ameipongeza Bodi, Menejimenti, wafanyakazi na wanachuo
wote wa TaSUBa kwa kazi kubwa wanayoiofanya kila mwaka ya kuandaa na kuendesha
Tamasha hilo kwa kipindi cha miongo mitatu na nusu mfululizo na kuwataka kutembea
kifua mbele kwa rekodi hiyo iliyotukuka ndani na nje ya nchi.
Mhe. Mwakyembe amesema kuwa lengo la Tamasha hilo ni pamoja na kutunza na
kuenzi sanaa na utamaduni wa mtanzania, kutengeneza jukwaa ambalo wanafunzi wa
TaSUBa wanalitumia kupima kiwango chao cha umahiri katika sanaa kwa mwaka,
kukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani ili
kuonyesha utajiri wao wa sanaa na utamaduni, pamoja na kutengeneza jukwaa
ambalo ni kiungo cha kujenga mahusiano ya wasanii wa ndani na nje ya nchi kupitia
maonyesho ya sanaa na kubadilishana uzoefu na uwezo katika kuendeleza tasnia ya
sanaa.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye amesema kuwa taasisi inajivunia mafanikio makubwa
wanayoendelea kuyapata kupitia tamasha hilo kwani kwa sasa tamasha linajumuhisha
wasanii wa ndani na nje ya nchi pamoja na wanafunzi waliosoma katika taasisi hiyo
miaka ya nyuma na waliopo mafunzoni.
Aidha Dkt. Makoye amewashukuru wakazi wa Bagamoyo kwa ushirikiano ambao
wamekua wakiuonyesha katika kushirikiana na Taasisi kuendeleza na kuthamini sanaa
na utamaduni wa mtanzania.
Naye Chifu wa Unyanyembe na Mwenyekiti wa Chama cha Machifu Tanzania Mhe.
Msagati Fundikira amewapongeza watendaji wa TaSUBa kwa kutoa wataalamu wazuri
katika fani ya sanaa na utamaduni kwani kwa ufanya hivyo wamekua wakiendeleza na
kudumisha utamaduni wa mtanzania kwa vizazi vya leo.
Tamasha hili la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa la Bagamoyo lenye kauli mbiu
isemayo “Sanaa na Utamaduni katika kupiga vita madawa ya kulevya” limeshirikisha
wasanii kutoka Kenya, Ufaransa, Uingereza, Zimbabwe na Mayyote na kuudhuriwa na
mabalozi mbalimbali akiwemo balozi wa Malawi, balozi wa Palestina, balozi wa
uholanzi, pamoja na wawakilishi kutoka ubalozi wa Zambia, Saudi Arabia, Msumbiji,
Japani, Ujerumani, Marekani, India, Shirikisho la Urusi, Angola na Kenya.
No comments:
Post a Comment