Meneja
wa kituo cha Nitetee Foundation, Johaness Emmanuel akipokea hundi ya
sh. 1,260,000 za malipo ya mchango wa uanachama wa bima ya afya kwa
watoto 25 wa kituo hicho kutoka kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya
Nyamagana, kulia mwenye kinasa sauti ni Mwenyekiti wa Taasisi ya The
Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania Sibtain Meghjee ambayo
imetoa fedha hizo kwa kituo hicho na Karibu Foundation.Kulia mwenye
shati ya draft ni Meneja Matekelezo wa NHIF Mkoa wa Mwanza Calistus
Mpangala. Picha ya Baltazar Mashaka.
Afisa
Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Mkoa wa Mwanza,
Castus Mpangala akitoa ufafanuzi wa huduma zinazotolewa na mfuko huo kwa
wananchi waliohudhuria semina ya bima ya afya iliyoandaliwa na Taasisi
ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania ili kuwahamasisha
kujiunga na mfuko huo kwa ajili ya kupata matibabu kwa gharama nafuu.
Semina hiyo ilifanyika jijini Mwanza.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongella mwenye kofia akiwa ameshika moja ya
mashuka yaliyotolewa msaada na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF)
Mkoa wa Mwanza kwa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe. Wa tatu kulia ni
Mganga Mkuu wa Mkoa Dk.Leonard Subi, Meneja wa mfuko huo mkoani Mwanza
Dk. Mohamed Kilolile wanne kulia na kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Uekerewe Estomiah Chang'a.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (mwenye kofia) hivi karibuni akinunua
samaki aina ya Furu kutoka kwa akinamama wachuuzi wa samaki katika Soko
la Kakukulu lililopo wilayani Ukerewe. Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa
wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.
Picha na Baltazar Mashaka.
NA BALTAZAR MASHAKA,MWANZA
TAASISI
ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) imekabidhi hundi mbili
zenye thamani ya zaidi sh. 2.5 kwa vituo vya Karibu Foundation na
Nitetee Foundation ili kuwawezesha watoto 50 wanaolelewa kwenye vituo
hivyo kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF).
Akizungumza
jana baada ya kukabidhi hundi hizo Mwenyekiti wa TD & CF Sibtain
Meghjee alisema fedha hizo zitatumika kugharamia matibabu ya watoto hao
kwa kipindi cha mwaka mmoja.
“
Watoto wanaolelewa kwenye vituo vya Nitetee Foundation na Karibu
Foundation, wengi wao wanatoka kwenye familia duni na wanaishi katika
mazingira magumu.Tumeona tuwasaidie kwa kuwakinga na magonjwa kwa
kuwalipia mchango wa uanachama wa Bima ya Afya wa sh. 54,000
utakaomuwezesha mtoto kutibiwa kwa mwaka mzima ambapo kila kituo
kimepewa sh. 1, 260,000 kwa ajili ya watoto 25 ambao wamesajiliwa
tayari, ”alisema.
Meghjee
alisema kuwa mbali na vituo hivyo taasisi Bilal Muslim Mission of
Tanzania pia itapewa msaada huo wa fedha sh. 1,260,000 kwa watu 50 wasio
na uwezo ili wajiuge na mfuko wa NHIF lakini pia The Deskk & Chair
nayo itawafadhili watu 50 kwa kuwalipia gharama matibabu kwenye mfuko
huo.
Hata
hivyo, alivishauri vyombo vya habari viteo fursa kwa kutangaza mambo
mazuri ya heri kwenye kurasa za mbele za magazeti badala ya kuwalisha
sumu wasomaji inayotokana na habari za migororo ambazo huchukua nafasi
kubwa kwenye kurasa za mbele za magazeti.
“
Mkituletea changamoto za wananchi tukazitatua kunairahisishia serikali
kuwafikia na itasaidia kuondoa hofu iliyopo baina ya serikali na
wananchi dhidi ya Uislamu maana sisi tunaamini uovu hauna nafasi kwa
dini yoyote.Niombe magazeti mambo mema na mazuri yatangazwe kwenye
kurasa za mbele badala ya mambo mabaya na ya migogoro tu,”alishauri
Meghjee.
Akizungumza
baada ya kupokea hundi hiyo Meneja wa Nitetee Foundation Johaness
Emmanuel alisema dhana yao ni kuendelea kuielimisha jamii katika ngazi
ya familia ili kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili kuwe na
jamii ya watu salama na Tanzania salama isiyo na vitendo vya ukatili.
“Ipo
dhana kuwa wamiliki wa vituo vya kulea watoto wanajinufaisha kupitia
vituo hivyo na vipo kwa maslahi binafsi badala ya watoto.Dhana hiyo ni
potofu na ndio maana tunapambana kwa kuelimishaa jamii kupitia
vipeperushi, magazeti na vipindi vya televiesheni ili tuwe na jamii ya
watu salama bila ukatili,”alisema Emmanuel.
Kwa
upande wake, Asumpta Ngatunga wa Karibu Foundation alieleza kuwa ili
kupunguza na kutokomeza ukatili wana mikakati ya kuendelea kuhamasisha
na kutoa elimu kwenye jamii ili kuoinga vitendo hivyo.
Aidha,
Meneja Matekelezo wa NHIF Mkoa wa Mwanza Calistus Mpangala asilimia 31
ya Watanzania wamejiunga na mfuko huo ingawa kuna changamoto za baadhi
ya watoa huduma kutowahudumia vizuri wanachama wa mfuko huo.
Alisema
NHIF iko mbioni kuajiri wataalamu watakaokuwa wakiratibu huduma
zinazotolewa kwenye baadhi ya vituo na hospitali zinazowahudumia
wanachama wa mfuko huo na kuhakikisha zinatoa huduma nzuri ili kuondoa
malalamiko.
Mpangala
aliongeza kuwa NHIF imeingia mkataba na watoa huduma mbalimbali ambao
malipoya madai yao hulipwa ndani ya siku 60 na hivyo lipo tatizo kwa
baadhi yao kuchelewesha madai yao ili yahakikiwe kabla ya malipo
kufanyika na hao ndiyo wanaotoa huduma mbaya kwa wanachama wa mfuko.
No comments:
Post a Comment