Sunday, September 3, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji wote nchini kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya viwanda mbalimbali katika maeneo yao. https://youtu.be/hiutkuE7nig

SIMU.TV: Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula amezionya halmashauri zinazoomba kujengewa nyumba na baada ya kujengewa wanazitelekeza. https://youtu.be/WPfeROm0uF4

SIMU.TV: Wanafunzi zaidi ya mia saba wa shule ya msingi Michiga B waliokuwa wakisomea kwenye vibanda vya nyasi wanatarajiwa kuondokana na adha hiyo ya ukosefu wa madarasa baada ya jeshi la ulinzi la wananchi Tanzania JWTZ kuamua kusimamia ujenzi wa madarasa ya shule hiyo. https://youtu.be/JTpVjvb3vRo

SIMU.TV: Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kesho itaanza kulipa fidia kwa wananchi wote watakaoguswa na mradi wa uboreshaji wa barabara na mifereji. https://youtu.be/7oGY52gUzNs

SIMU.TV: Wakulima wa kanda ya kati wameshauriwa kulima zao la korosho kama zao mbadala kwa kuwa zao hilo linahimili mabadiliko ya tabia ya nchi. https://youtu.be/fBnOR-pZFNA

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Mbarali kwa kujadili vizuri hoja za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali CAG. https://youtu.be/xeHNlVHwe1Q

SIMU.TV: Wazazi na walezi wameshauriwa kuwa na utaratibu wa kuwasiliana na walimu ili kuweza kufuatilia maendeleo ya taaluma ya mtoto awapo shuleni. https://youtu.be/NtaXLsUPL7w

SIMU.TV: Kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi maliasili na utalii imesema itaishauri serikali namna ya kumaliza mgogoro wa ardhi katika kitongoji cha Uvinje na hifadhi ya Saadani wilayani Bagamoyo. https://youtu.be/jHvZyCTGZxw

SIMU.TV: Uelewa mdogo wa wananchi katika uandaji na upangaji wa nyaraka za miradi ya maendeleo umeelezwa kuwa ni changamoto inayokwamisha wananchi kushiriki katika kupanga mipango ya maendeleo. https://youtu.be/2XZ_3_3gZrM

SIMU.TV: Bodi ya wadhamini  ya TFF jana imekutana na viongozi wajuu wapya wa shirikisho la soka TFF ili kufahamiana na kupanga mipango mipya. https://youtu.be/GeVWICCPpUc

SIMU.TV: Klabu ya soka ya Simba leo imecheza mchezo wa kirafiki na timu ya Hard Rock kutoka Pemba ambapo Simba imeibuka na ushindi wa mabao matano kwa bila. https://youtu.be/FBqDC54KUKQ

SIMU.TV: Wadau na wapenzi wa soka katika manispaa ya Mtwara Mikindani wamelalamikia uchakavu wa uwanja wa Nangwanda Sijaona hali inayo hatarisha maisha ya mashabiki. https://youtu.be/cDG5XEGK22I

SIMU.TV: Uongozi wa mkoa wa Morogoro umewakamata raia wawili wa China na kuwaamuru kurejea kwao baada ya kukiuka mara kadhaa maagizo ya serikali; https://youtu.be/e7un7IZwXr8

Mkazi mmoja aliyejenga katika hifadhi ya barabara mjini Musoma amesababisha ukosefu wa maji baada ya kukataa kupitisha bomba katika eneo lake; https://youtu.be/pY8tGZU6jZs

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam Paul Makonda amewataka wananchi watakaopitiwa na mradi wa maendeleo ya mkoa kutumia vizuri fidia zao; https://youtu.be/tSQ9X73ZAOA

SIMU.TV: Zaidi ya shilingi milioni 200 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa visima vya kuvuna maji katika hospitali ya Kagondo wilayani Muleba; https://youtu.be/IgwpKpFbL54

Mkuu wa mkoa wa Geita Ezekiel Kyunga amesema viongozi wa dini wana wajibu wa kuhubiri amani ili watu waweze kuachana na imani potofu; https://youtu.be/cHuGTxTx-6M

SIMU.TV: Baadhi ya wakulima wa zao la Korosho mkoani Tabora wameiomba serikali kuwapatia mbegu bora za zao hilo ili kuongeza uzalishaji; https://youtu.be/kxNlezXQPTY

SIMU.TV: Mwenyekiti wa bodi ya TGNP Mtandao Vicensia Shule amesema kuwa kuwepo kwa madawati ya jinsia katika taasisi mbalimbali kumesaidia kupunguza ukandamizaji; https://youtu.be/6xEF0egO8Iw

SIMU.TV: Mlinzi wa kati wa timu ya taifa Abdi Banda amewaomba watanzania kuiunga mkono timu hiyo kwani wamejipanga kuipatia sifa inayostahili; https://youtu.be/OQnykT3fHPk

SIMU.TV: umla ya timu 32 zimethibitisha kushiriki mashindano ya vijana katika wilaya ya Kinondoni yenye nia ya kukuza na kuendeleza vipaji; https://youtu.be/F8vGV2nBaS0

SIMU.TV: Vijana kote nchini wamehimizwa kujifunza mchezo wa Gofu ili waweze kujipatia ajira lakini pia kuweza kuweka fiti afya zao; https://youtu.be/-bMpwJeV-FY

SIMU.TV: Mashindano ya mpira wa Kikapu ya Kilimanjaro Cup yamezinduliwa rasmi mkoani Kilimanjaro ambapo timu kadhaa zinatarajia kushiriki; https://youtu.be/28Ra6ssDfS0

No comments: