Sunday, September 3, 2017

BANDARI YA TANGA YANG’ARA KILIMANJARO CUP

Mchezaji wa timu ya Bandari Tanga akiruka juu kuwania mpira wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kilimanjaro Cup yanayoendelea kwenye viwanja wa KCMC na Baptist ambapo mechi hiyo ilikwisha kwa Bandari Tanga kuibuka na ushindi wa vikapu 64 dhidi ya 57 
Wachezaji wa timu za Bandari Tanga na Baptist wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kilimanjaro Cup yanayoendelea kwenye viwanja wa KCMC na Baptist ambapo mechi hiyo ilikwisha kwa Bandari Tanga kuibuka na ushindi wa vikapu 64 dhidi ya 57 
Kocha wa timu ya Bandari Tanga Mohamed Fazal akitoa maelekezo kwa timu hiyo wakati wa mapumzikokulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu 
Kocha wa timu ya Bandari Tanga,Mohamed Fazal akitoa mawaidha kwa timu hiyo wakati wa mapumziko kulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu 
Kikosi cha timu ya Mpira wa Kikapu ya Bandari Tanga 


TIMU ya Mpira wa Kikapu ya Bandari Tanga ambayo inashikilia Ubingwa wa Mashindano ya Kilimanjaro Cup mwaka jana inashiriki tena Mashindano hayo kutetea ubingwa huo mwaka huu katika mashindano yanayoendelea kwenye viwanja KCMC mjini Moshi.

Kitendo cha timu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo kwa mara nyengine kinaonyesha namna kinavyotumia vema fursa hiyo kuitangaza Bandari ya Tanga.

Katika kuhakikisha suala hilo linakwenda kwa vitendo leo timu ya Bandari Tanga wameibuka na ushindi wa vikapu 64-57 dhidi ya timu ya Baptist katika mechi iliyokuwa na upinzani mkubwa huku Bandari Tanga ikipambana ili kuhakikisha inatetea Ubingwa wake na kuondoka na ushindi huo.

Awali akizungumza wakati akizundua mashindano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira amezitaka timu shiriki kutumia fursa ya mashindano hayo kutangaza utalii wa nchi ikiwemo mlima Kilimanjaro.“Baada ya mashindano haya timu zote shiriki zitakwenda kupanda mlima Kilimanjaro ili kuweza kuhamasisha wanamichezo na wananchi wengine kuweza kutalii mlima huo “Alisema Mkuu huyo wa mkoa.

Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana kuchangia damu kwa wahitaji ambapo katika viwanja hivyo sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kuchangia damu kwa hiari.Mashindano hayo yanaendelea kwa wiki nzima katika viwanja vya Baptist na KCMC Mkoani Kilimanjaro.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments: