MSANII wa muziki wa kizazi kipya Shaban Mpute 'Ne-Mo' amesema amedhamiria kurudi katika
familia ya muziki kivingine, huku akitarajia kuachia wimbo wake mpya
unaitwa 'Kipotabo'Septemba 19 mwaka huu ambayo imetengenezwa katika
studio za Combination Sound chini ya mtayarishaji Man Water na
video kutengenezwa na Kwetu Studio.
Akizungumzia
ujio wake mpya Ne-Mo chini ya lebo ya 'Digital City Drimz' alisema
kuwa amedhamiria kuirejesha RnB ya Bongo katika viwango na pia kuipeleka
nje ya mipaka ya Tanzania, kwa sababu anahifahamu vizuri na kwa sasa
kuna wasanii kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Navy Kenzo
na wengineo wameubeba muziki wa Bongofleva na kusaidia kuupenyeza
kimataifa, naye ana matumaini makubwa ya kufika walipo wasanii hao.
Ne-mo
ujio wake utakuwa wa aina yake na Watanzania hawatajutia kumsubiri
Ne-Mo arudi kwa muda wote huo, kwamba ukimya wake umetokana na masomo
ambapo aliamua kutulia amalizie masomi kisha aendelee na Harakati za
Muziki na alikuwa masomoni akiwa amesomea masuala ya 'Mass
Communication' na anaeleza kuwa sasa ametulia na amepata 'Mameneja '
ambao wanamsimamia na kumrejesha kwa kishindo katika muziki.
"Nimejipanga
vuzri pamoja na mameneja wangu narudi kimuziki kikweli kweli, naomba
mashabiki wa muziki Tanzania wanipokeekwa mara nyinyingine, nilitoka
kidogo kwenda masomini lakini sasa nimerudi rasmi katika muziki"alisema
Ne-mo.
Alisema
kwa upande wa mtindo wa Rap na Hip Hop mwanzoni mwa miaka ya 2000
Profesa Jay alichangia kuuweka muziki wa Hip Hop mtaani na kukubalika na
kila kundi la jamii., miaka michache iliyopita waliibukakina Child Benz
na Nako 2 Nako ambao walisaidia kujenga misingi ya kuufanya muziki wa
Hip Hop kukubalika kibiashara.
Alisema
sasa hivi wasanii kama Weusi, Darasa, Billnas, Young Dee na kadhalika
ambao wanauwekea vionjo muziki wa Rap kufanya kupenya zaidi na hata
uanze kuimbwa na hata akina dada ambao zamani ilikuwa ni nandra kuwa na
mapenzi na muziki wa Rap.
Meneja
wa mwanamuziki huyo Habibu Anga 'Guru Picasso' alisema kuwa siku ya
Jumatatu wataachia rasmi wimbo wa Kipotabo wa msanii huyo na
amekuja kuitikisa zaidi Tanzania na Afrika Mashariki kama ilivyotokea
mwaka 2013 alipoachia wimbo uliokwenda kwa jina la "Number One" ambao
alimshirikisha mkali mwenzake 'Ommy Dimpoz' wimbo ambao ulikuwa mkubwa
na kugeuka kama 'wimbo wa Taifa' kama wasemavyo mtaani.
Baada
ya mafanikio makubwa ya wimbo huu wa 'Number One' Ne-Mo hakuwahi kutoa
kazi yake nyingine yoyote ile, zaidi ya nyimbo za kushikishwa ambazo ni
'Mrs Superstar' ya Young Killer, 'Tulikuwepo' ya Niki Mbishi, 'Sijutii'
ya Msamiati na nyinginezo nyingi.
No comments:
Post a Comment