Friday, September 22, 2017

MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA KWENYE DVD PEMBA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limemkamata mwanamke mwengine akiwa na jumla ya kete 969 zinazosadikiwa kuwa ni madawa ya kulevya zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya DVD.

Mwanamke huyo ambaye amekamatwa na wenziwe wawili wanaume katika maeneo ya PBZ Chake Chake anakuwa wa pili kukamatwa ndani ya kipindi cha wiki mbili baada ya Septemba 9 mwezi huu kukamatwa mwengine akiwa na jumla ya kete 3621.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Madungu Chake Cheke Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shikhan Mohamed Shikhan amemtaja mwanamke huo ni Asha Mohamed Issa (30) mkaazi wa Wawi Chake Chake, huku wenzake wakiwa ni Ali Nyoro Tirima (32)wa Wawi na Salim Said Kombo 23 mkaazi wa Konde Wilaya ya Micheweni.

Aidha Kamanda Shikhan amesema jeshi la polisi Mkoa wa Kusini Pemba tayari inayo majina ya mabaharia wanaofanya kazi katika meli zinazotoka Unguje kuelekea Pemba wanaotumiwa kusafirisha madawa ya kulevya na kuwataka kuacha vitendo hivyo kwani jeshi hilo linawafuatilia.

“Ni kwamba wito wangu kwa mabaharia wa meli zinazotoka Unguja kuja Pemba, tayari tunayo majina ya mabaharia wa meli zote MV Mapinduzi, meli za Bakhresa zote hao ndio ambao wanatoa msaada mkubwa kwa waleta madawa ya kulevya yanapita katika mikono yao,tunawajua na tunawafuatilia kwa karibu”

Aidha kamanda huyo amewawata amewataka wamilika wa makampuni kuwatahadharisha mabaharia wao, kuacha kutumiwa na wahalifu wa madawa ya kulevya wa bangi na unga wanaopeleka madawa ya kulevya kisiwani humo kwani watawakamata.

Kwa upande mwengine Kamanda Shekhan amewaonya wanawake wanaojiingiza kufanya biashara za madawa ya kulevya kuacha kabisa biashara hizo na kutafuta nija halali za kujipatia kipato.

“Kweli huyu ni mwanamke wa pili kumkamata kwa mkoa wetu, lakini natoa wito kwa wanawake hiyo sio biashara ya kusema wanaweza wakapata utajiri , warudi nyuma watafute biashara zinazokwenda na maadili ya biashara” Septemba 9 mwaka huu jeshi la Polisi Mkuu wa Kusini Pemba huko maeneo ya Mkoani Pemba ilifanikiwa kumkamata na kete 3621 Zuhura Ahmed Ali (29) wa Jadida na alifikiswa mahakamani kwa mara ya kwanza Septemba 14
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shikhan Mohamed Shikhan akizungumzia kukamatwa kwa madawa hayo.
Mzigo wa madawa hayo

No comments: