Saturday, August 5, 2017

WAKULIMA WAHIMIZWA KUTUMIA RASILIMALI ZA NCHI KWA KULIMA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe akisoma na kupata maelezo mbalimbali kuhusu ufanisi katika Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe akisikiliza maelezo ya namna ya ufyatuaji matofali yanayotumika kujengea nyumba za NHC mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe (Kushoto) akisikiliz akwa makini maelezo kuhusu ufanyaji kazi katika banda la TAMISEMI mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango.
Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara kuu ya kilimo Ndg Twahir Nzallawahe akisikiliza maelezo mbalimbali katika banda la Nanyamba mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara kuu ya kilimo Ndg Twahir Nzallawahe akisikiliza maelezo mbalimbali katika banda la Nanyamba mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.


Na Mathias Canal, Lindi

Pamoja na mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima nchini Tanzania lakini wametakiwa kujikita zaidi na kilimo cha mazao yanayostahimili ukame ikiwemo kuanzisha kilimo cha umwagiliaji hususani katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa Bahari ya Hindi katika Mikoa ya Mtwara na Lindi.

Kufanya hivyo ni kutumia vizuri rasilimali za nchi ikiwemo maji na maeneo oevu katika kilimo chenye tija jambo ambalo linatoa fursa kwa wakulima wadogo kuwa na kipato kikubwa na kutafsiri ipasavyo kipato cha nchi na mtu mmoja mmoja.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara kuu ya kilimo Ndg Twahir Nzallawahe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Nzallawahe alisema kuwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi serikali tayari imeanzisha kanda ya umwagiliaji ambapo kuna mradi wa Kitele huku akisema kuwa jitihada zaidi za kuwa na miradi ya umwagiliaji katika mikoa yote nchini zinaendelea.

Alisema kuwa pamoja na mbinu bora za Kilimo Mifugo na Uvuvi wanazopatiwa wananchi lakini pia Maonesho ya Nanenane kwa mwaka huu 2017 yamezidi kuwa bora zaidi ukilinganisha na Maonesho ya kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kutembelea katika Maonesho hayo ili kujifunza mbinu mbalimbali za Kilimo Mifugo na Uvuvi huku akiwasisitiza zaidi kununua bidhaa zinazotengenezwa na kuzalishwa ndani ya nchi kwani kufanya hivyo watarahisisha kipato cha wakulima nchini ikiwemo pia kurahisisha kasi ya ukuaji wa kilimo.

Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya nchini hususani kuwapatia wananchi maeneo kwa ajili ya kilimo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango alisema kuwa Katika Maonesho haya wakulima watajifunza mbinu bora za kisasa za kilimo zitakazowawezesha kupata mazao mengi na kuinua kipato chao.

Aidha ametoa wito kwa wakulima na mashirika kujitokeza katika maonesho hayo kwa sababu watapata fursa ya kujifunza mambo mengi na kubadilishana uzoefu na wataalamu mbalimbali wa kilimo.

No comments: