Wafanyakazi
watano wa Wizara ya Fedha na Mipango (Walioketi) waliopatiwa udhamini
wa masomo nchini katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa kiwango cha
Shahada ya Uzamili uliotolewa na Shirika la Maendeleo la Uingereza
(UKAID-DFID), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa
British Council-Tanzania ambao ndio waratibu wa Program hiyo ya miaka
mitano, itakayogharimu Shilingi bilioni 3.6 kwa lengo la kuongeza ujuzi
na umahili wa rasilimali watu katika masuala ya uchumi, mipango,
usimamizi wa fedha za Umma na Sheria za kimataifa. Kutoka kushoto
Harieth Lubinga, John Kabiti, Susan Mbayuwayu, Peter Kalugwisha na
Gloria Mduda.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia)
akiongea ofisini kwake na Mkurugenzi Mkazi wa Idara ya Kimataifa ya
Maendeleo kutoka Serikali ya Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy,
kuhusu masuala mbalimbali ukiwemo ufadhili wa miaka mitano wa Taasisi
hiyo wa masomo ya juu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo
katika ngazi ya Shahada ya Uzamili.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb)
(kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb) (kushoto), wakielekea katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa
ufadhili wa miaka mitano wa masomo ya juu kwa watumishi wa Wizara ya
Fedha na Mipango, uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza wenye thamani
za shilingi bilioni 3.6.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia),
Mkuu wa Shirika la Msaada la Uingereza (UKAID) nchini Tanzania Beth
Arthy (wa pili kushoto) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.
Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (kushoto) wakielekea katika uzinduzi wa
program ya miaka mitano ya mafunzo ya mafunzo ya juu kwa ngazi ya
Shahada ya Uzalimili kwenye vyuo vikuu nchini Uingereza kuhusu masuala
ya uchumi, mipango, usimamizi wa fedha umma na sheria kwa baadhi ya
watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango uliotolewa na Serikali ya
Uingereza.
Mkurugenzi
Mkazi wa British Council, Bi. Angela Hennelly, akizungumza jambo wakati
wa uzinduzi wa mradi wa miaka mitano wa ufadhili wa masomo ya juu
katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya
Fedha na Mipango kwenye vyuo vikuu mbalimbali nchini Uingereza kupitia
Shirika la Maendeleo la UKAID-DFID utakaogharimu shilingi bilioni 3.6.
British Council Tanzania ni waratibu wa mpango huo.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb)
akizungumza katika uzinduzi wa program ya miaka mitano ya mafunzo kwa
ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la
UKAID-DFID, uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango,
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza
jambo wakati wa uzinduzi wa program ya ufadhili wa masomo ya Juu katika
vyuo vikuu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na
Mipango katika ngazi ya shahada ya uzamili kupitia ufadhili wa Shirika
la Maendeleo la Uingereza UKAID-DFID wenye thamani ya shilingi bilioni
3.6, Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na viongozi
waandamizi wa UKAID-DFID, British Council-Tanzania, Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, na watumishi wa Wizara ya
Fedha na Mipango walionufaika na ufadhili huo (kushoto) wakifurahia
baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mpango wa miaka mitano wa ufadhili wa
masomo kwa ngazi ya shahada ya uzamili katika vyuo vikuu vya nchini
Uingereza katika Nyanja za uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za umma
na sheria za kimataifa uliotolewa na Serikali ya Uingereza kwa Wizara
hiyo.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia),
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza
(UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa
British Council, Bi. Angela Hennelly na Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (wa pili kulia) wakiwa
katika picha ya pamoja na Maafisa wa Serikali na Watumishi wa Wizara ya
Fedha na Mipango waliopata ufadhili wa Mafunzo kutoka UKAID-DFID, muda
mfupi baada ya kuzindua rasmi program hiyo, Jijini Dar es Salaam. (Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)
No comments:
Post a Comment